Journal matin

Habari za asubuhi za siku ya pili tarehe 13/06/2023

  • Imepita mwaka mmoja hadi leo, tarehe kumi na tatu mwazi wa sita mwaka huu tunao , mji wa Bunagana ulipochukuliwa na  waasi wa M23 na wafuasi wao wa Rwanda.
  • "Natoa wito kwa wananchi kuunga mkono  maono ya Rais wa  Nchi ambaye anajitahidi kwa ajili ya  hali ya usalama nchini, na ninaalika  makundi yote yenye silaha kuweka chini silaha zao kwa ajili ya kurejesha amani na usalama. >>. Huu ni ujumbe wa Waziri wa Ulinzi wa inchi la Kongo ya Kidemokratia, Jean Pierre Bemba, aliyewasili jana  mjini Goma.
  •  
  • Katika jimbo la  Ituri, yapata  watu makumi inne  na watano waliuawa na watu wenye silaha  usiku wa siku ya mungu  katika eneo la wakimbizi  la LALA karibu na kituo cha biashara cha BULE , karibu  kilomita mia moja kaskazini mwa Bunia katika mtaa wa Djugu.
  • Katika jimbo la  Kivu ya  Kaskazini, shambulio jipya lililohusishwa na waasi wa ADF usiku wa siku ya mungu  liliua watu wanane huko Kasindi, mji ulioko kilomita makumi mnane kutoka mji wa Beni.
  • Jimboni  Kasai, mashirika ya kiraia yamelaani hali ya  ukosefu wa usalama kwa mwezi mmoja sasa huko Tshikapa.
  • Jimbo la   Kivu ya Kusini linakumbwa na janga la kipindupindu kwa siku chache sasa. Kuzuka kwa visa vya kipindupindu ambavyo vinazingatiwa zaidi katika maeneo matatu ya afya ya mji Bukavu.
  • Jimboni  Tanganyika, usimamizi wa kesi zinazoshukiwa za kipindupindu unaendelea katika eneo la afya la Kiambi, mtaani Manono.
  • Katika mtaa wa Beni, zaidi ya wakaaji  elfu kenda wa kijiji cha Samboko karibu kilomita makumi sita  kutoka Beni wamekosa  usaidizi wa kiafya kwa miaka mitano./sites/default/files/2023-06/130623-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3