Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi 

  • Jimboni  Kivu ya Kaskazini, mapigano yalifanyika jana siku mzima kati ya wanajeshi wa FARDC na waasi wa M23 kwenye pande mbili katika maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo.
  • Majadiliano  ya awali ya mchakato wa amani wa Nairobi ya tatu: rais wa zamani wa Kenya aliyechaguliwa  kuwa mpatanishi wa mchakato wa Nairobi na jumuiya ya Afrika ya  Mashariki, alipokeya jana  viongozi  wa  kisiasa  wa inchi la Kongo Kongo na wawakilishi wa jumuiya tofauti  kutoka Kivu ya Kaskazini, Kivu  ya Kusini na Ituri.
  • Habari kuhusu mzozo  uliopo mjini Kinshasa kuhusu vikwazo vya silaha: wakati  baadhi ya vyama vya siasa na vikundi vya raia vikipanga kuandamana dhidi ya Jumuiya ya Kimataifa kuhusu suala hilo,  waziri ahusikaye na  Mambo ya Nje amewaonya wananchi dhidi ya hatua zozote zitakazomsaidia adui wa Kongo. Katika mahojiano  na Radio Okapi kutoka Luanda nchini Angola aliko, Christoph Lutundula anafasiria tena  matamshi yake yaliyotafsiriwa vibaya sikun ya tano  iliyopita kuhusu kuzuiwa kwa  inchi kupata silaha. Kulingana naye inchi ya Kongo haiko tena chini ya vikwazo rasmi.
  • Katika jimbo la  Kivu ya Kaskazini, eneo la afya ya  Nyiragongo linatangaza  kuenea kwa visa vya malisho mbaya katika maeneo mbalimbali ya wahami . Malisho mbaya hiyo  huathiri zaidi watoto kutoka miezi sita hadi miezi makumi tano  na kenda  pamoja na wajawazito.
  • “Kisukari: kuelimisha ili kulinda maisha yajayo” hii ndiyo ndiyo mada ya sherehe ya siku kuu duniani   ya kupinga ugonjwa huu mwaka huu inayosherekewa kila tarehe kumi na inne mwezi wa kumi na mmoja .
  • Katika jimbo la Kivu Kusini, maporomoko ya udongo  yamesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi mmoja vibaya katika mji wa Bukavu.
  • Kunaripitiwa Vifo viwili kufuatia kutoroka  kwa wafungwa   wa gereza kuu la Gbadolite siku ya mungu . Viongozi wanasikitika kwamba zaidi ya wafungwa makumi mnane  walifanikiwa kutoroka katika gereza hiyo  ambayo haina vyoo bora.
  • Wizi wa kila mara  wa viombo via   SNCC kwenye sehemu ya reli ya barabara ya Kindu – Kongolo – Kabalo katika jimbo la Tanganyika. Ni Kiongozi wa kituo cha SNCC huko Kongolo ndio alitangaza habari siku ya mungu  .
  • Kuwasili Mbuji-Mayi jana  hii, huko Kasaï-Oriental, kwa ujumbe wa Mfuko ya Kitaifa kuhusu masuala ya pori  /sites/default/files/2022-11/151122-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3.