Journal Soir

Habari za siku ya tano jioni 

  • "Vita vilivyowekwa juu yetu na majirani zetu vinaomba kujitolea kwa  kila mmoja wetu. Ni wakati wa kunyamazisha tofauti zetu za kisiasa ili kutetea sote kwa pamoja, nchi yetu mama. Maneno haya yanatoka kwa Mkuu wa Nchi Felix Antoine Tshisekedi wakati wa hotuba yake kwa taifa jana Alhamisi, tarehe tatu Novemba.
  • Jimboni Kivu  ya Kaskazini, siku ya tano hii ni siku ya saba mfululizo ya kukaliwa na waasi wa M23 wa mji mkuu na miji maeneo makubwa ya tarafa la Rutshuru.
  • Kivu Kaskazini: Vizuizi sita vimewekwa kwenye barabara mbalimbali katika tabaka Kamuronza, usultani wa Bahunde katika tarafa la Masisi.
  • Jimboni Kivu ya  Kaskazini, Mtandao wa Haki za Kibinadamu, REDHO, unaonyesha wasiwasi wake kwa kuzuka upya kwa kesi za mauaji wakati wa maandamano ya umma yaliyoandaliwa na vuguvugu la kiraia na ma groupe de pression huko Butembo.
  • Kivu ya Kaskazini, shirika la raia la tabaka Banande Kainama katika tarafa  la Beni linapinga hatua yoyote ya kuitaka serikali ya Kongo kukomesha operesheni ya pamoja ya FARDC-UPDF inayoendelea katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.
  • Jimboni Kwilu, kufatana na ukatili unaohusiana na ukosefu wa usalama wa Kwamouth huko Mai-Ndombe, kijiji kimoja kimeshambuliwa hii siku ya ine tarehe tatu Novemba mwaka tunao katika tarafa la Bagata na waasi  wenye silaha.
  • Katika jimbo la Tshopo, mkaguzi mkuu mpya wa kijeshi wa majimbo ya Tshopo, Bas-Uélé na Haut-Uélé anatoa wito kwa mahakimu wa kijeshi kuheshimu maagizo ya uongozi na sheria.
  • Katika jimbo la   Ituri, sare mia moja makumi mbili na tano na gilet za kujikinga, na vyengine vifaa, zilikabidhiwa kwa polisi wa kitaifa wa Kongo huko Ituti hii siku ya inne./sites/default/files/2022-11/04112022_-p-s-journalswahilisoir-00_web.mp3