Habari za siku ya kwanza jioni
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, operesheni ya lipiza ushuru kwa gari ilianza katika mji wa Goma hii siku ya kwanza.
- Mtaani Beni, msimamizi wa oparesheni za kudumisha na kurejesha utulivu wa umma kwa polisi wilayani alitangaza hii siku ya kwanza mbinu mpya ya operesheni za polisi, ile ya kufanya kazi na FARDC katika operesheni za pamoja kwa lengo la kuweka usalama katika miji iliyo chukuliwa na jeshi.
- Siku mbili baada ya kutoroka kwa karibu wafungwa mia mbili kutoka gereza kuu la Matadi, mfumo wa mashauriano wa mashirika ya kiraia wa Kongo Central unahofia kuzuka upya kwa ukosefu wa usalama.
- Katika jimbo la Maniema, gereza kuu la Kasongo limerekodi tena kifo kingine kimoja wikendi hii.
- ''Fanya afya ya akili kwa wote kuwa kipaumbele cha kimataifa''. Hii ndiyo mada ya Siku ya Afya ya Akili Duniani mwaka huu inayoadhimishwa tarehe kumi mwezi wa kumi Oktoba.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, zaidi ya wakuu watano wa masomo wa baadhi ya shule kubwa kubwa za mji wa Goma wamesimamishwa kazi kwa muda kulingana na kisheria.
- Kazi za ujenzi wa kilomita sita za barabara ya kitaifa namba mbili kati ya mji wa Bukavu na uwanja wa ndege wa Kavumu zinaendelea kawaida.
- Kitika jimbo la Kasai-Oriental, wiki moja baada ya kuwashwa umeme mjini kwa saa chache, Mbuji-Mayi imerudi tena gizani./sites/default/files/2022-10/10102022_-p-s-journalswahililundisoirparfloridakahambu-00_web_.mp3