Habari za siku ya tano jioni
- Katika jimbo la kwilu, watu wanne wamefariki miongoni mwa watu waliokimbia mzozo kati ya wa Teke na wa Yaka kutoka eneo la kwamouth huko maindombe .
- Kulifunguliwa jana hapa mjini Kinshasa Mkutano wa sita wa shirika la Wabunge wa Afrika wanaohusika na Ulinzi na Usalama .
- Jimboni ituri, kiongozi wa operesheni za pamoja ya FARDC na jeshi la Uganda UPDF na makamu wake walijilekeza katika eneo la Boga.
- Katika mtaa wa Beni, shirika ya kiraia ya eneo la Banande-Kainama inapendekeza doria ziongezwe katika vijiji vya Banande Kainama
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, baraza la vijana la mtaa wa Eringeti lilianzisha tangu siku ya kwanza iliyopita, kazi ya kusisimua vijana kwa lengo la kujitahidi kwa kutafuta amani katika eneo hili.
- Waziri anayehusika na elimu, Tony Mwaba anatangaza kwa wakongomani wote kwa jumla na haswa kwa wanafuzni waliofaulu kwenye mtihani ya serikali ya mwaka wa elfu mbili na kumi na tano kwamba vieti via mwisho wa shule za sekondari vinapatikana kwenye chumba kikuu kienye kuhusika na shule za msingi na sekondari.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, muungano ya wakaadji wa Kongo wanaofanya kazi bila malipo ASVOCO, unamuomba rais wa Jamhuri ya Kidemokratia ya Kongo kuanzisha kazi yakuboresha sheria .
- Kampuni nne za uchimbaji madini zilikwenda jana kwenye Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, ofisi ya Lubumbashi kuzungumzia hali ya maisha ya watoto.
- Mjini Goma, siku ya pili iliyopita, hospitali kuu ya jimbo la Kivu ya Kaskazini iliweza kufanya upasuaji yakuachanisha mapacha wawili waliokuwa wakikamata kwa miezi miwili tangu kuzalika./sites/default/files/2022-10/071022-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3