Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni 

  

  • Rais wa Jamhuri na kamanda Mkuu wa Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Polisi wa Kitaifa wa Kongo, Felix Antoine Tshisekedi aliongoza hii siku ya ine katika makao makuu ya FARDC katika Kambi ya Kokolo sherehe za mabadiliko ya uongozi wa jeshi  kati ya Jenerali wa jeshi wa FARDC anayemaliza muda wake. 
  • Jimboni Ituri, hali ya usalama inaimarika polepole lakini kwa hakika katika maeneo kadhaa ya tarafa la Djugu na kwenye barabara ya kitaifa namba makumi mbili na saba
  •  Mjini  Goma, polisi wa mjini wanasema walikamata angalau magunia kumi na tatu  ya bangi na masanduku mnane ya dawa ambazo muda wake wa matumizi umeisha.
  • “Tunataka amani. Mwende  mukafanye bidii ili turudi kuishi nyumbani kwetu, Bunagana”. Hivi ndivyo wasichana wa Bunagana, wakimbizi walio katika maeneo ya RWASSA 1, RWASSA 2 NA RUGABO, walivyojieleza siku ya pili pa Rutshuru-Kati, mbele ya baadhi ya wafanyakazi wa kibinadamu walioenda kusherehekea nao Siku ya Kimataifa ya Msichana.
  • Jimboni Kasaï-Oriental, wanafunzi kadhaa wanaosoma katika shule zilizo karibu na barabara za Fatshi na Salongo, katika manispa Kanshi na Bipemba, wamekuwa wakishambuliwa na vijana wahalifu kwa tangu karibu wiki tatu sasa.
  • Katika Jimbo la Kwilu, Kardinali Fridolin Ambongo, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Kinshasa akiwa katika ziara ya kichungaji katika mji wa Bandundu tangu siku ya pili iliyopita, alisoma misa ya amani na upatanisho wa wakaaji wa Kwamouth katika jimbo hilo la  Maindombe jioni ya siku ya tatu tarehe kumi na mbili mwaka tunao.
  • Katika jimbo la Kivu Kusini, Tume ya Haki na Amani ya Dayosisi ilikutanisha wadau wote katika mchakato wa uchaguzi ili kujadili changamoto zinazohusiana na uchaguzi uliopangwa kufanyika Desemba mwaka kesho nchini Kongo.
  • Mjini Beni, angalau viongozi makumi mbili  wa mashirika mbalimbali ya vijana, vuguvugu la wananchi na vyama vya wanawake walihamasishwa hii siku ya tatu dhidi ya kuchezewa,  na kuungana huduma za usalama./sites/default/files/2022-10/13102022-p-s-journalswahilijeudisoir-00_web_.mp3