Habari za siku ya tatu jioni
- Miili makumi mbili na saba, watu makumi tatu na mbili ambao wamekosekana na karibu watu makumi sita walionusurika, hii ni tathmini kwa sasa ya kuzama kwa boti ya ICCN iliyotokea usiku wa kuamukiya siku ya pili iliyopita huko Mbandaka kwenye mto Kongo.
- Mjini Goma, hali ya wasiwasi inapungua mchana wa hii siku ya tatu kwa saa za baada ya saa sita katika jiji zima.
- Mchungaji Jean Omari Ramazani wa Kanisa la Eglise chrétienne pour toutes les nations, anayejulikana sana mjini humo, yuko mbele ya mahakama tangu hii siku ya tatu katika mahakama ya kijeshi ya Goma.
- Meja Jenerali Dick Olum ndiye kamanda mpya wa wanajeshi wa Uganda waliotumwa DRC katika operesheni ya pamoja na FARDC dhidi ya ADF inayoitwa "Shujaa".
- Visa vingine viwili vya vifo vilirekodiwa siku ya kwanza tarehe kumi na siku ya pili tarehe kumi na moja mwezi wa kumi mwaka tunao miongoni mwa wakimbizi waliotoka Kwamouth, ambao kwa sasa wanaishi katika jimbo la Kwilu.
- Kongo Central ni jimbo wa majaribio wa operesheni ya utambuzi wa kibayometriki kwa wafanya kazi wa serikali katika majimbo.
- Mjini Mbuji Mayi, jimboni Kasai-Oriental, kuligunduliwa sehemu kubwa ya vifaa vya kupambana na malisho mabaya.
- Huko Nord Ubangi, takriban watu elfu kumi katika eneo la afya la Gumba-Lego, kilomita makumi ine na tano kutoka Yakoma-Kati, hawajui tena wapi pa kwenda ili kupata matibabu.
- Barua ya ombi ya Watu wanaoishi na Ulemavu, iliwasilishwa siku ya pili tarehe kumi na moja oktoba, kwa Waziri Mkuu.
- Kituo cha uchunguzi wa Volcano OVG cha Goma, kinatangaza kwamba kimegundua shughuli isiyo ya kawaida iliyorekodiwa siku ya pili kwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi katika maeneo yake ya uchunguzi ya Munigi na Kibati katika tarafa la Nyiragongo./sites/default/files/2022-10/12102022_-_p-s-journalswahilimercredisoir-00_web_.mp3