Journal matin

Habari za siku ya tatu asubuhi 

  • Mahakama ya Wakaguzi wa hesabu iliwasilisha hii siku ya pili ripoti yake kuhusu utekelezaji wa bajeti ya 2021 katika ofisi ya Bunge la Kitaifa.
  • Jimbo la Kivu ya Kusini lina matatizo ya kibajeti tangu miaka mitatu sasa. Mkuu wa mkoa anakemea wizi wa fedha za serikali unaofanywa na baadhi ya wasimamizi wa huduma.
  • Katika jimbo la TSHOPO, barabara ya Kisangani-Ubundu iko katika hali mbaya sana. 
  • Jimbo l’Ituri limepewa mpango wa uendeshaji wa shughuli za upokonyaji silaha, uondoaji wa silaha na mpango wa kurejesha katika jamii na uimarishaji.
  • Kardinali Fridolin Ambongo alifika hii siku ya pili tarehe kumi na moja oktoba kwa mara ya kwanza kabisa pa Bandundu, mji mkuu wa jimbo la Kwilu.
  • Mjini Kinshasa, zaidi ya watu mia tatu, wengi wao wakiwa vijana, walikamatwa, wakiwemo mia moja kumi na wawili waliofungwa.
  • Ulimwengu unasherekea hii siku ya pili Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike.
  • "Binti wa Beni anahitaji utulivu, usaidizi na kusindikizwa ili kustawi." Haya ndiyo tunayoweza kujifunza kutoka shughuli nyingi zilizo andaliwa katika mji wa  Beni hii siku ya pili, katika kusherekea mwaka wa kumi wa Siku ya Kimataifa ya Msichana./sites/default/files/2022-10/12102022-p-s-journalswahilimercredimatin-00_web.mp3