Habari za siku ya kwanza asubuhi
- Malipo ya mishahara ya wanajeshi wa kikosi cha jumuiya ya inchi za Africa mashariki, EAC kilichotumwa mashariki mwa inchini Kongo: ni kila nchi ambayo inawajibika kwa mishahara, vyakula na vifaa vyote vya wanajeshi wake waliotumwa nchini Kongo.
- Katika jimbo la Mai - Ndombe, hali ya utulivu inaonekana huko tangu karibu wiki mbili sasa katika eneo la Kwamouth ambako mapigano ya kikabila yalizuka karibu miezi mbili iliyopita, na kusababisha vifo vya watu
- Kuhusu hali ya Bandundu, Raisi Félix-Antoine Tshisekedi aliwaagiza baadhi ya wajumbe wa serikali kupitia huduma zao maalum, kuandika makosa katika eneo lote linalohusika na eneo la migogoro la Kwamouth.
- Jimboni Kivu Kusini, zaidi ya watu elfu makumi tatu na saba mia tano walichunguzwa kiafya kuhusu matatizo ya afya ya akili katika kipindi cha miezi sita ya kwanza ya mwaka tunao.
- Siku ya mungu , tarehe kenda mwezi wa kumi mtihani wa kuajiri wa mahakimu ulifanyika katika eneo lote la kitaifa.
- Rais wa Jamhuri alihimiza wikendi hii, Waziri Mkuu kuchukua hatua zote muhimu ili jukumu la utengenezaji wa machapisho yote ya thamani, kama vile diploma, passports na vinginevyo, lirudi kwa uhakika na kwa kipekee kwa Benki Kuu ya Kongo.
- Kwa wakongomani wanaotaka kwenda kuishi Marekani, kumbuka kuwa masharti ya kucheza bahati juu ya DV Loterry ya mwaka wa elfu mbili ishirini na ine yamepunguzwa kwa kiasi fulani./sites/default/files/2022-10/101022-p-s-journalswahililundimatin_web_.mp3