Habari za siku ya pili asubuhi
- Waziri wa Kongo aneyehusika na Haki za Binadamu anasema kwamba inchi ya Kongo imejitolea kabisa kwa kukuza haki za binadamu kwa mtazamo kamili.
- Katika jimbo la Kwilu, ma adui wawili wanaodaiwa kuhusika na mauaji ya wakuu wa vijiji vya BUKUSU na FADIAKA, waliokamatwa katika eneo la Bagata walipelekwa siku ya kwanza mjini Bandundu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kasakazin, Msemaji wa operesheni za kijeshi Sokola ya kwanza anatoa wito kwa wakaadji wa Butembo na eneo zima kuwa waangalifu ili kupambana na tishio la kigaidi .
- Katika jimbo la Kivu ya Kusini … kuliandaliwa siku ya pili hii siku bila kazi yoyote katika mtaa na mji wa Uvira na vile vile katika mji wa Sange.
- Huko Ituri, vituo saba vya redio za jamii katika mtaa wa Mambasa, karibu kilomita mia moja makumi sita na tano kutoka mji wa Bunia, vimepewa vifaa vya mawasiliano na shirika lisilo la kiserikali la Search For Common Ground.
- Inchi ya Kongo ya Kidemokratisa inakuwa kwa sasa sawasawa na Indonesia na Brazili katika mkakati wa kugombea haki za wakazi wake.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Prince Kihangi, mwanabunge jimboni anapendekeza mtaa wa walikale ushurutishwe na mradi wakupewa mkopo wa kaboni .
- Jimbo Kivu Kusini, kilalo cha muda cha Cihanda katika eneo la Nyangezi mtaani Kabare kilizinduliwa siku ya pili/sites/default/files/2022-10/051022-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web_0.mp3