Journal Soir

Habari za siku ya tano jioni ya tarehe 23/06/2023

  • Maaskofu wa Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo CENCO Jamuhuri wanaalika wakongoami wote kuwa makini . Pia wanashutumu ukosefu wa usalama na kutokuvumiliana kisiasa miezi michache kabla ya uchaguzi
  • Amri mpya ya kutokutoka nje ilitolewa katika jimbo lote la Kwango kila siku kuanzia ya mbili za usiku  hadi saa kumi na mbili za asubuhi.
  • Mkutano ya mashirika inne inapangwa kufanyika siku ya pili ijayo mjini Luanda katika inchi la Angola kuhusu mzozo kati ya Jamuhuri yaKidemokratia ya Kongo  na Rwanda.
  •  Shirika lisilo la kiserikali la Journaliste en danger  kwa kushirikiana na internews waliandaa kikao ya uchunguzi  ya mbinu  za ufuatiliaji na taratibu za ulinzi wa wapashahabari.
  • Jimboni Ituri,  mbuga la wanyama la Okapi linalaani upotevu wa zaidi ya hekta mia  nne za nafasi yake kufuatana na shughuli za kibinadamu.
  • Katika jimbo la Maniema, Meya wa mji wa Kindu alianza jana siku ya inne  huko Kindu kazi yakubomoa majengo yasiyoheshimu kanunu.
  • Jimboni Kivu ya Kusini, zaidi ya wanafunzi makumi inne  kutoka Kalehe hawajui jinsi ya kufanya  mitihani katika vyuo vikuu vyao vya Bukavu.
  • Katika jimbo la Kwilu, zaidi ya walimu makumi kenda  wa shule  kumi na moja  za msingi za mji wa Bandundu wanashutumu kutolipwa kwa malipo yao  kwa muda wa miezi sita ambayo ni franga  elfu  makumi tano yakikongomani pamoja na garama za uendeshaji za shule zao ./sites/default/files/2023-06/230623-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3