Habari za siku ya pili jioni ya tarehe 13/06/2023
- "Mashambulizi na kulipiza kisasi ya baadhi ya wanamgambo wa makundi yenyi kumiliki silaha huko Ituri ambao wanataka kuzarahu mchakato wa amani unaoendelea ndio msingi wa mauwaji za hivi karibuni katika eneo la Djugu". Haya ndiyo yale ambayo liwali wa jimbo la Ituri, Luteni Jenerali Johnny Luboya Nkashama, aliambia waandishi wa habari siku ya pili hii , siku moja baada ya mauaji ya raia makumi inne na sita katika eneo la wakimbizi la LALA.
- Jimboni Ituri, mzozo ulipunguka siku yab pili asubuhi katika kituo cha Bule baada ya maandamano ya vijana kukemea mauaji ya watu makumi inne na sita siku ya kwanza katika eneo la wakimbizi la LALA katika mtaani Djugu.
- Kuhusu tu Mauaji ya mara kwa mara katika majimbo ya Ituri na Kivu ya Kaskazini, Mwanabunge Jackson Ausse anaarifu zaidi ya watu makumi inne na watano waliouawa na wanamgambo tangu tarehe tano hadi kumi na tatu mwezi wa sita huu.
- Baada ya mauaji haya ya Lala , lawama, shutumu na husuni hutoka kila mahali. Kwa mufano Unicef, MONUSCO, umoja wa ulaya, na Ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
- Hali ya wasiwasi ya usalama katika ilikuwa mada ya mazungumzo, siku ya pili hii huko Goma, kati ya Waziri wa Ulinzi, Jean-Pierre Bemba Gombo, na viongozi wa kidini wa jimbo la Kivu Kaskazini.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shughuli zote zilianza tena siku ya pili hii huko Kasindi-Lubiriya, mji unayopatikana katika mtaa wa Beni , karibu kilomita makumi mnane na tano kaskazini mashariki mwa mji wa Beni. Kulingana na duru zetu, maduka, shule, biashara ndogo ndogo na shughuli nyingine hufanyika kama kawaida katika eneo hilo la mpakani na Uganda.
- Katika jimbo la Kongo central , hebu tuzungumze juu furaha hii ya wafanyabiashara wa chakula huko Boma. Boti mbili zilizobeba zaidi ya tani elfu sita za vyakula vibichi zilifika siku ya kwanza katika bandari ya Kuntuala terminal .
- Mawasiliano yamekatika kwa zaidi ya miaka miwili kati ya eneo la Beni na uchifu wa Walese-Vonkutu katika jimbo la Ituri. Kilalo moja ililounganisha maeneno haya mawili ilipelekwa na maji ya mvua. Wanainchi wanaomba kukarabatiwa kwa kilalo hiki ya umuhimu wa wa kiuchumi na usalama katika eneo hili.
- Siku kuu ulimwenguni ya kupinga utumikishwaji wa watoto. Mjini Lubumbashi, shirika ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na offisi ya Masuala ya Kijamii na baadhi ya washirika wao walienda siku ya kwanza katika mtaa wa Rwashi mjini Lubumbashi ili kuahamasisha wazazi kuwatoa watoto wao kwenye maeneo ya uchimbaji madini./sites/default/files/2023-06/130623-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3