Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 12/06/2023
- Katika jimbo la Ituri, yapata watu makumi inne na watano waliuawa na watu wenye silaha usiku wa siku ya mungu katika eneo la wakimbizi la LALA karibu na kituo cha biashara cha BULE , karibu kilomita mia moja kaskazini mwa Bunia katika mtaa wa Djugu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shambulio jipya lililohusishwa na waasi wa ADF usiku wa siku ya mungu liliua watu wanane huko Kasindi, mji ulioko kilomita makumi mnane kutoka mji wa Beni.
- Jimboni Kasai, mashirika ya kiraia yamelaani hali ya ukosefu wa usalama kwa mwezi mmoja sasa huko Tshikapa.
- Jimbo la Kivu ya Kusini linakumbwa na janga la kipindupindu kwa siku chache sasa.
- Jimboni Tanganyika, usimamizi wa kesi zinazoshukiwa za kipindupindu unaendelea katika eneo la afya la Kiambi, mtaani Manono.
- Katika mtaa wa Beni, zaidi ya wakaaji elfu kenda wa kijiji cha Samboko karibu kilomita makumi sita kutoka Beni wamekosa usaidizi wa kiafya kwa miaka mitano.
- Ni lazma kupanda miti katika mji wa Bukavu. Ni hivi ndivio Waziri Gilbert Kabanda, akiwa moja wa wakuu wa mji huu, alisema kwa wakazi wa Kivu ya Kusini, wakati ya mazungumzo yao./sites/default/files/2023-06/120623-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3