Habari za jioni 23 Aprili, 2025
- Kinshasa : Mahakama ya katiba iliendeleza vikao vyake hii siku ya tatu tarehe makumi mbili na tatu Aprili mjini Kinshasa katika Kesi ya Bukanga-Lonzo. Washtakiwa Matata Ponyo Mapon, Déogratias Mutombo na Christho Grobler hawakufika kila mmoja kwa sababu yake binafsi
- Doha : Mazungumzo kati ya serikali ya Kongo na waasi wa AFC/M23 huko Doha, inchini Qatar, yamekwama. Ujumbe wa waasi uliondoka huko hii siku ya pili kurejea katika mji wa Goma
- Kinshasa : Profesa Yves Mudimbe Yoka amefariki dunia hii siku ya pili nchini Marekani. Ni mmoja wa waandishi wakubwa wa vitabu inchini Kongo na duniani./sites/default/files/2025-04/230425-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3