Habari za jioni 02 Aprili, 2025
- Bandundu : Uchaguzi wa mkuu wa mkoa na maseneta katika jimbo la Kwilu, unafanyika hii siku ya tatu katika Bunge la Jimbo la Kwilu mjini Bandundu
- Bunia : Chama cha mawakala wa forodha walioidhinishwa nchini Kongo (ACCAD) kimeshutumu Ofisi ya Udhibiti wa Kongo (OCC) huko Ituri kukusanya ushuru kinyume cha sheria katika forodha ya Mahagi tangu miaka kumi sasa
- Beni : Huko Kivu Kaskazini, uratibu wa mashirika ya kiraia wa Beni, Butembo na Lubero unakataa wazo la uondoaji wa vikosi vya Uganda (UPDF) katika tarafa la Lubero.