Journal Soir

Habari za jioni 28 Februari, 2025

  • Kinshasa : Zaidi ya watu elfu nane mia tano  tayari wamezikwa tangu kukaliwa kwa mji wa Goma na waasi wa M23. Waziri wa afya ya umma, daktari Roger Kamba alitoa takwimu hizi wakati wa mkutano na waandishi wa habari ulioandaliwa hii siku ya ine na mwenzake wa Mawasiliano na vyombo vya habari, Patrick Muyaya
  • Kinshasa : Mjini Kinshasa, kongamano kuhusu kutokomeza ugonjwa wa polio litakafanyika kuanzia tarehe ine hadi tarehe sita Machi  ijayo chini ya uandalizi wa Wizara ya afya ya umma 
  • Kindu : Jimbo la Maniema liko gizani tangu zaidi ya siku kumi sasa kufuatana na mgomo wa wafanyakazi wa SAKIMA wa Kalima wanaodai kulipwa mishahara yao ya miezi kadhaa, mkurugenzi wa mkoa wa shirika la umeme la taifa SNEL Maniema anasema./sites/default/files/2025-02/280225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3