Habari za jioni 04 Februari, 2025
- Kinshasa : Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) wameanza mfululizo wa mashauriano na wadau wakuu nchini kwa lengo la kuwasilisha mradi wao wa kumaliza mgogoro kupitia mapatano ya kijamii ya amani na kuishi pamoja
- Kinshasa : Jean-Marc Kabund, mkuu wa chama cha Alliance pour le Changement, hajafunguliwa kutoka gerezani. Guylain Mwandji mshauri wa kitaifa wa chama hicho ndiye amethibitisha hayo, akijibu kwa video iliyosambaa mitandaoni kwamba tayari amefunguliwa
- Kananga : Huko Kasai-Central, wafanyakazi na watendaji wa Kurugenzi Kuu ya Mapato ya Kasai-Central, DGRKAC, waliofukuzwa kazi kwa amri mpya ya liwali, wamekasirishwa na kufukuzwa kazi, wanasema wamefukuzwa bila sababu./sites/default/files/2025-02/040225-p-s-journalswahilisoir-00-web.mp3