Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 29/07/2024
- Usafiri ulikuwa ngumu siku ya kwanza hii hapa mjini Kinshasa. Madereva wa tekso waliaandaa mgomo ili kukemea unyanyasaji unaofanywa na polisi na huduma nyingine za serikali.
- Kuhusu matukio katika uwanja wa Martyrs wakati wa mkutano kati ya mwimbaji wa nyimbo za kumtukuza mungu Mike Kalambay na wakazi wa Kinshasa, ambapo watu kenda walifariki na wengi kuumia siku ya sita hapa mjini Kinshasa. Kulingana na mwanamke ambaye alishiriki katika mkutano ni tabia mbaya ya ki megendo ya wa polisi ndio msingi wa matukio haya.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, utulivu ilionekana siku ya kwanza hii katika kijiji cha Ngoliba, kati ya miji ya Nyange na Bibwe, eneo la Bashali Mokoto, mtaani Masisi.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini tuwajulishe kwamba kuna Watoto ambao wamekuwa wasimamizi wa familia zao ambao lazima wachunge na kuwalisha kaka au dada zao wadogo.
- Katika eneo la Beni jimboni Kivu ya Kaskazini, Kampuni ya Vihumbira (SSV), ambayo inafanya kazi ya ukarabati wa barabara ya Butembo-Manguredjipa na ujenzi wa barabara ya Manguredjipa-Bandulu, ina wasiwasi kuhusu hali ya usalama katika eneo hilo.
- Katika jimbo la Kasai ya mashariki, huko ambako tumejulishwa kwamba Mradi wa kupata maji na usafi wa mazingira wa PASEA utatekelezwa hivi karibuni huko .
- Katika jimbo la Kasai-Central, moto uliitokeza mwishoni mwa juma lililopita kwenye bandari ya Ilebo kwenye Kampuni ya Kitaifa ya Reli, SNCC.
- Huko Ituri, Shirika la Biashara la Kongo FEC -ITURI, linakaribisha pendekezo la Rais wa Jamhuri Felix Tshisekedi la kupunguza ushuru kwa waendeshaji uchumi katika jimbo la Ituri./sites/default/files/2024-07/290724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3