Habari za siku ya pili jioni tarehe 16/07/2024
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mapigano mapya yametokea siku ya pili hii asubuhi kati ya jeshi la Kongo na waasi wa m23 karibu na barabara ya Bweremana-Shasha kusini mwa mtaa wa Masisi.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini kuzorota kwa hali ya kiuchumi, kijamii na kibinadamu, kutokana na ukosefu wa usalama, katika mji wa Goma na mazingira yake ni mada cha majadiliano huko Goma kati ya waziri mkuu makamu wa Mambo ya Ndani na usalama na watu mbalimbali wa jamii na siasa mjini Goma.
- Waziri Mkuu makamu wa Ulinzi Guy Kabombo aliwasili siku ya pili hii huko Kikwit, katika jimbo la Kwilu.
- Askofu Mkuu wa Kisangani anasema amefurahishwa na matokeo ya kazi yake ya Mkuu wa Baraza la Maaskofu la Kitaifa la Kongo CENCO.
- Jimboni Kasai Oriental, visa vichache vya uhalifu vimerekodiwa siku hizi katika mji wa Mbuji-Mayi.
- Katika jimbo la Tanganyika, kutoroka kwa wafungwa wote kutoka gereza kuu la Manono wakati wa usiku wakuhamkiya siku ya kwanza.
- Huko Ituri, watu wawili wanandoa waligunduliwa wamefariki siku ya kwanza katika kijiji cha Bandundundu mtaani Mambasa.
- Mjini Kalemie, washahuri wa mitaa wanashutumu hali duni ya kazi. Wanatangaza kuwa hakuna ushirikiano mzuri kati yao na viongozi wa mitaa .
- Katika jimbo la Kasai-Oriental, liwali wa jimbo hafurahi na kazi ya ukarabati ya barabara ya kitaifa Namba mmoja , ya Mbuji Mayi - Mwene-Ditu katika sehemu yake kati ya eneo la Bena hadi Lukalaba./sites/default/files/2024-07/160724-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3