Habari za siku ya inne jioni tarehe 11/05/2023
- Jimboni Ituri, wanafunzi mia moja kutoka mtaa wa Djugu waliweza kufanya mitihani ya kwanza ya serikali kupitiya msaada wa askari wa MONUSCO.
- Katika jimbo la Maindombe, mitihani ya kwanza ya serikali ya mwaka huu imepangwa kwa sehemu katika mtaa wa Kwamouth. Wanafunzi kadhaa hawakushiriki kutokana na hali mbaya ya usalama ambayo imesalia hapo.
- Jimboni Kivu ya Kusini, kuhusiana na ajali ya mafuriko ya nvua ya Kalehe, serikali la jimbo inatoa wito wa usaidizi wa jumla kwa ajili ya waathiriwa.
- Siku bila kazi mjini Uvira katika jimbo la Kivu ya Kusini… Karibu waandamanaji elfu moja, wakiwemo wavuvi, akina mama wanauzisha samaki kutoka ziwa na watu wengine, waliandamana siku ya siku ya inne hii .
- Kufungwa kwa uvuvi katika nchi nne za pembezoni ni moja ya hatua nyingine nyingi zilizochukuliwa katika mradi wa LATAFIMA, mradi wa usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Tanganyika.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, eneo la afya la Lubero na lile la Mangurijipa hazina gari lakuchukuwa wagondjwa kwa dharura.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, tuwajulishe kwamba zaidi ya wanawake mia mbili wahami wamefaidika na huduma salama ya uzazi katika eneo la Bulengo kwa muda wa siku makumi tatu zilizopita
- Majenerali wawili wa jeshi na polisi wafikishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Kijeshi mjini Kinshasa./sites/default/files/2023-05/110523-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3