Habari za siku ya tatu jioni tarehe 10/10/2024
- Baraza kisheria ya inchi, yani Conseil d’Etat lilichunguza kesi makumi tatu na kenda siku ya tatu hii hii kuhusu kufutwa kwa kura za wagombea wa ubunge makumi mnane na wawili .
- Tume ya haki na amani ya dayosisi ya Maniema inaomba tume huru ya taifa ya uchaguzi, CENI kutambua na kuwaihazibu wafanyaka kazi wake waliotoa vifaa vya uchaguzi kwa wagombea walioondolewa kwenye oroza ya wagombea.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, kamati ya usalama jimboni inatangaza hatua zinazolenga kukabiliana na uhalifu, ambao umekuwa ukiongezeka katika wiki za hivi karibuni katika mji wa Goma.
- Huko Ituri, idadi ya mifugo imepunguka kwa kiasi kikubwa kufuatia kuendelea kwa ukosefu wa usalama katika jimbo hili. Wafugaji wengi wamehamisha ng'ombe wao hadi jimbo jirani ya Haut Uélé.
- Huko jimboni Kasai-Central , Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, CNDH inatoa wito kwa serikali kuu kutoa fedha kwa haraka ili kuharakisha kutumwa kwa mahakimu katika maeneo ya mahakama.
- Inchi ya Kongo na hiyo ya Arabie Saoudite zatia saini mkataba wa makubaliano katika sekta ya madini.
- Wakazi wa wilaya ya Kinsuka-pecheurs , katika mtaa wa Ngaliema, wamekuwa bila makao kwa zaidi ya wiki tatu./sites/default/files/2024-01/100124-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3