Journal matin

Habari za siku ya tatu asubuhi ya tarehe 14/06/2023

  • Mauaji, ubakaji na uhalifu mwingine wa kivita mashariki mwa Kongo yakidemokratia. Haya ni maneno ya shirika yakutetea haki za kibinadamu  Human Rights watch kuelezea ugumu wa maisha ya wakongomani wanaoishi katika sehemu ya nchi inayokaliwa na waasi wa M23 na wasaidizi  wao wa Rwanda.
  • Hali ya wasiwasi ya usalama katika  ilikuwa  mada ya mazungumzo,  siku ya pili hii huko Goma, kati ya Waziri wa Ulinzi, Jean-Pierre Bemba Gombo, na viongozi  wa kidini wa jimbo la  Kivu Kaskazini.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, watumiaji wa sehemu ya barabara ya Beni-Butembo wanaomba kupelekwa kwa vikosi vya ulinzi na usalama kwenye barabara hii huu  inayokabula miji hii miwili ya jimbo la Kivu ya Kasajazini.
  • "Mashambulizi na kulipiza kisasi ya  baadhi ya wanamgambo wa  makundi  yenyi kumiliki silaha huko Ituri ambao wanataka kuzarahu  mchakato wa amani unaoendelea ndio msingi wa mauwaji  za hivi karibuni katika eneo la Djugu". Haya ndiyo yale ambayo liwali  wa jimbo la Ituri, Luteni Jenerali Johnny Luboya Nkashama, aliambia waandishi wa habari  siku ya pili hii , siku moja baada ya mauaji ya raia makumi inne na sita katika eneo la wakimbizi  la LALA.  
  • Jimboni Ituri, mzozo ulipunguka  siku yab pili asubuhi katika kituo cha Bule baada ya maandamano ya vijana kukemea mauaji ya watu makumi inne  na sita siku ya kwanza  katika eneo la  wakimbizi la LALA katika mtaani Djugu
  • Kuhusu tu Mauaji ya mara kwa mara katika majimbo ya Ituri na Kivu ya Kaskazini, Mwanabunge Jackson Ausse anaarifu zaidi ya watu makumi inne  na watano waliouawa  na wanamgambo tangu tarehe tano hadi kumi na tatu mwezi wa sita huu.
  • Baada ya mauaji haya ya Lala , lawama,  shutumu na husuni  hutoka  kila mahali.  Kwa mufano Unicef,  MONUSCO, umoja wa ulaya,  na Ubalozi wa Marekani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Mashirika haya yote na washirika wa kimataifa wanashutumu na  kulaani shambulio hili dhidi ya kambi ya wakimbizi  huko Ituri.
  • Katika jimbo la Kongo central , hebu tuzungumze juu  furaha hii ya wafanyabiashara wa chakula  huko Boma. Boti mbili zilizobeba zaidi ya tani elfu sita za vyakula vibichi zilifika siku ya kwanza   katika bandari ya Kuntuala terminal .
  • Mawasiliano yamekatika kwa zaidi ya miaka miwili kati ya eneo la Beni na uchifu wa Walese-Vonkutu katika jimbo la Ituri. Kilalo moja ililounganisha maeneno haya mawili  ilipelekwa  na maji ya mvua. Wanainchi  wanaomba kukarabatiwa kwa kilalo hiki ya  umuhimu wa wa kiuchumi na usalama katika eneo hili./sites/default/files/2023-06/14062023-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3