Habari za asubuhi za siku ya pili tarehe 13/06/2023
- Imepita mwaka mmoja hadi leo, tarehe kumi na tatu mwazi wa sita mwaka huu tunao , mji wa Bunagana ulipochukuliwa na waasi wa M23 na wafuasi wao wa Rwanda.
- "Natoa wito kwa wananchi kuunga mkono maono ya Rais wa Nchi ambaye anajitahidi kwa ajili ya hali ya usalama nchini, na ninaalika makundi yote yenye silaha kuweka chini silaha zao kwa ajili ya kurejesha amani na usalama. >>. Huu ni ujumbe wa Waziri wa Ulinzi wa inchi la Kongo ya Kidemokratia, Jean Pierre Bemba, aliyewasili jana mjini Goma.
- Katika jimbo la Ituri, yapata watu makumi inne na watano waliuawa na watu wenye silaha usiku wa siku ya mungu katika eneo la wakimbizi la LALA karibu na kituo cha biashara cha BULE , karibu kilomita mia moja kaskazini mwa Bunia katika mtaa wa Djugu.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, shambulio jipya lililohusishwa na waasi wa ADF usiku wa siku ya mungu liliua watu wanane huko Kasindi, mji ulioko kilomita makumi mnane kutoka mji wa Beni.
- Jimboni Kasai, mashirika ya kiraia yamelaani hali ya ukosefu wa usalama kwa mwezi mmoja sasa huko Tshikapa.
- Jimbo la Kivu ya Kusini linakumbwa na janga la kipindupindu kwa siku chache sasa. Kuzuka kwa visa vya kipindupindu ambavyo vinazingatiwa zaidi katika maeneo matatu ya afya ya mji Bukavu.
- Jimboni Tanganyika, usimamizi wa kesi zinazoshukiwa za kipindupindu unaendelea katika eneo la afya la Kiambi, mtaani Manono.
- Katika mtaa wa Beni, zaidi ya wakaaji elfu kenda wa kijiji cha Samboko karibu kilomita makumi sita kutoka Beni wamekosa usaidizi wa kiafya kwa miaka mitano./sites/default/files/2023-06/130623-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3