Habari z'asubuhi 05 Februari, 2025
- Kinshasa : Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC) wameanza mfululizo wa mashauriano na wadau wakuu nchini kwa lengo la kuwasilisha mradi wao wa kumaliza mgogoro kupitia mapatano ya kijamii ya amani na kuishi pamoja
- Kinshasa :Daktari Denis Mukwege anaomba mauaji ya watu wa Kongo yakomeshwe na kulaani ukimya wa jumuiya ya kimataifa kufuatana na hali hii. Alisema hayo hii siku ya pili
- Kananga : Huko Kasai-Central, wafanyakazi na watendaji wa Kurugenzi Kuu ya Mapato ya Kasai-Central, DGRKAC, waliofukuzwa kazi kwa amri mpya ya liwali, wamekasirishwa na kufukuzwa kazi, wanasema wamefukuzwa bila sababu./sites/default/files/2025-02/050225-p-s-journalswahilimatin-00-web.mp3