Habari za siku ya pili asubuhi tarehe 16/07/2024
- Waziri Mkuu makamu wa Mambo ya Ndani na usalama Jacquemain Shabani alikomesha jana ziara yake ya kazi ya siku mbili katika mji wa Butembo jimbini Kivu ya Kaskazini
- Mji wa Beni huko jimboni Kivu la Kaskazini, licha ya miaka mingi ya vita na ukatili, licha ya ukombizi ya mara kwa mara ya watu wanaokimbia ukosefu wa usalama katika mazingira yao, maisha hakika sio ya kupendeza, lakini yapo.
- Katika jimbo la Kivu Kaskazini, mapigano kati ya jeshi la Kongo na washirika wake kamundi yenyi silaha zidi ya waasi wa M23 yaliripotiwa siku ya kwanza hii katika maeneo kadhaa ya mtaa wa Masisi.
- Huko jimboni Ituri, wanasiasa wawili: Danny UNYITHOWUN na UPAR DÉSIRE, walikamatwa huko Mahagi kisha kuhamishwa siku ya pili hadi Kinshasa na shirika ya kijasusi ya raia.
- Katika jimbo la Haut-Uélé, muungano ya mashirika ya kiraia inaeleza wasiwasi wake kuhusu uchimbaji wa dhahabu unaofanywa na vyama vya ushirika vinavyosaidiwa na wataalamu wa China na wengine katika maeneo ya uchimbaji madini katika jimbo hili.
- Jimboni Maniema, daktari mkurugenzi wa hospitali kuu ya Lubutu anatangaza kesi za ungondjwa unaosabishwa na nyama yaani Monkeypox katika eneo hilo.
- Katika jimbo la Kivu Kaskazini: maeneo yote makumi matatu na inne na za afya katika jimbo hilo hazina tena dawa ya ugonjwa ya kifua kikuu kwa zaidi ya wiki tatu sasa.
- Katika jimbo la Kivu ya kusini: Mgogoro katika kituo cha utafiti wa Lwiro unafikia siku yake ya tano siku ya kwanza hii./sites/default/files/2024-07/160724-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3