Journal matin

Habari za siku ya tano asubuhi  tarehe 12/07/2024

  • Majeshi ya jamuhuri ya kidemokratia ya Kongo FRADC yanaishutumu Rwanda kwa kutokuheshimu  mapatano ya kibinadamu yaliyotangazwa na  Marekani.
  • Mkuu makamu wa jeshi la FARDC anayesimamia ujasusi  aliwasili  siku ya inne hi huko mjini Beni jimboni Kivu ya Kaskazini, kwa ziara ya kazi.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini,  harakati ya wakimbizi wanaorejea katika vijiji vyao  inazingatiwa katika mtaa wa Rutshuru.
  • Katika jimbo la Ituri, kamati  za wakimbizi zinashutumu kutokuadhibiwa kwa wahusika wa mauaji ya zaidi ya watu mia moja kwa zaidi ya mwaka mmoja katika maeneo ya Savo na Benza katika mtaa Djugu.
  • Kiwango cha ugondjwa cha kisukari miongoni mwa watoto kinapunguka kulingana na utafiti unaofanywa hivi sasa na Mpango wa Kitaifa wa Kisukari katika hospitali ya watoto ya Kalembelembe hapa  Kinshasa.
  • Dola za Marekani milioni makumi mbili ni fedha ambao  mpango  wa Elimu uitwao Education Can no wait (ECW)", Mfuko wa Umoja wa Mataifa uliokusudiwa kwa elimu ya watoto wanaoishi katika hali ngumu , itaitoa kwa miaka mitatu ijayo nchini Kongo . 
  • Usumbufu katika  kanisa Kuu la Katoliki la Kinshasa. Shirika liitwao (ACKIN) linashutumu kile linachoeleza kuwa ni usimamizi mbaya unaofanywa na Kadinali Fridolin Ambango mkuu wa kanisa jimboni .
  •  Kanuni mpya  seneti zilikubaliwa siku ya tatu .Ilikuwa wakati wa kikao cha mashauriano ambako  maseneta makumi mnane  waliohudhuria walichagua kanuni hizo. 
  • Huko Kivu ya Kusini, wahanga wa mafuriko katika eneo la Katashola katika mtaa wa Kalehe ambao walipoteza paa za makao yao pia wanakabiliwa na shida ya ukosefu wa chakula.
  • Katika jimbo la Kasai Oriental:  kusimamishwa  siku ya tatu mjini Mbuji Mayi, kwa shughuli zote za ujenzi wa nyumba zilizofanywa kwenye eneo la Mitembela zinazoleta mzozo kwa miezi kadhaa kati ya Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Bakuanga MIBA na wanamemba  wa Chama cha BURP./sites/default/files/2024-07/120724-p-s-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3