Journal matin

Habari za siku ya inne asubuhi tarehe 11/01/2024

  • Baraza kisheria ya  inchi, yani Conseil d’Etat  lilichunguza kesi  makumi tatu na kenda  siku ya tatu hii hii kuhusu kufutwa kwa kura  za  wagombea wa ubunge  makumi mnane na wawili .
  • Habari kuhusu hatua yakuruhusu shiria kumfata  liwali  wa mji wa Kinshasa. Ofisi ya Gentiny Ngobila inataja  baadhi ya hali  usio halali unaohusu  hatua hii.
  • Tume ya haki na amani ya dayosisi ya  Maniema inaomba  tume huru ya taifa ya uchaguzi, CENI kutambua na kuwaihazibu  wafanyaka kazi  wake waliotoa vifaa vya uchaguzi kwa wagombea walioondolewa kwenye oroza ya wagombea.
  • Katika jimbo la  Kivu ya Kaskazini, kamati ya usalama jimboni  inatangaza  hatua zinazolenga kukabiliana na uhalifu, ambao umekuwa ukiongezeka katika wiki za hivi karibuni katika mji wa Goma.
  • Huko Ituri, idadi ya mifugo imepunguka kwa kiasi kikubwa kufuatia kuendelea kwa ukosefu wa usalama katika jimbo hili. Wafugaji wengi wamehamisha ng'ombe wao hadi jimbo  jirani ya Haut Uélé.
  • Huko jimboni Kasai-Central , Tume ya Kitaifa ya Haki za Kibinadamu, CNDH inatoa wito kwa serikali kuu kutoa fedha kwa haraka ili kuharakisha kutumwa kwa mahakimu katika maeneo ya mahakama.
  • Inchi ya Kongo na hiyo ya Arabie Saoudite  zatia saini mkataba wa makubaliano katika sekta ya madini.
  •  Wakazi wa wilaya ya Kinsuka-pecheurs , katika mtaa wa Ngaliema, wamekuwa bila makao  kwa zaidi ya wiki tatu./sites/default/files/2024-01/110124-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3