Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.
” KAMPENYI YA UCHAGUZI YENYI KURUHUSIWA NA SERKALI NI NINI, NA KAMPENYI YA UCHAGUZI KWA USIKIVU YA WOTE NI NINI ? ”
* Karine, mbele ya akujibu kwa swali lako, inafa tukumbushe kama uchaguzi ni kitendo charn rahiya kwakuchagua viongozi ao wasimamizi wake kwa kila daraja ya maisha ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.Uchaguzi ni kitendo ambacho kila mwanainchi wa inchi fulani ao mwanamemba wa kundi fulani anajulisha maoni yake wakati wa uchaguzi ao wakati wakuchukua hatua fulani.Uchaguzi ni pia uchunguzi wa taifa kwa jumla,wa rahiya wakongomani juu ya kuchagua wakuu viongozi vyake na kuchagua pia maandiko aoa maoni huenda kuongoza inchi wakati wa jamuhuri ya tatu. Kura ni kitendo cha upekee na hakiwezi kufanyika kwa kumtuma mtummwengine ao kwa njia ya barua.
Kwakurudilia ulizo lako Karine,kwa kuchungua veme .tunaweza kujulisha kama kampenyi ya utetezi kuhusu uchaguzi ni mda mwenyi kutangulia uchaguzi, wakati ambao vyama vya siasa na wakandidenti wanajitetea, nikusema wanawahubilia rahiya ili wawachague kwa uwingi.Ni lazima Karine , kutofaitisha kampenyi yenyi rn kuruhusiwa na serkali na kampenyi kwa usikivu wa jumla.
Kampenyi yenyi kuruhusiwa na serkali ni mda ambao wakandidenti wanajijulisha kwa njia televbijenina redio na kupitia magazeti,yale yote yakifata sheria yenyikuelekea uchaguzi.Wakandidentiwote wanapshwa kupewa mda sawa kwa kujitetea kwa njia ya redio ,televijeni, Na yale yote yanachunguliwa na Haute Autorite des medias,katika jamuhuri ya kidemokrasia ya kongo, inayao mipangoyake na sheria kuhusu jamabo lile.
ili liheshimiwe.
Kampenyi ya uchaguzi ya kiserkali,kufatana na sheria na nukta 28 ya sheria sifuru, sita kistari sifuru sifuru ya tarehe kenda mwezi wa tatu mwaka wa 2006, sheria yenyi kuelekea matayarisho ya uchaguzi katika jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kuhusu uchaguzi wa uraisi wajamuhuri , wateule wabunge la taifa na lile la majimbo , la miji mikubwa , komini na ya malokaliti,kampenyi yaani utetezi wa uchaguzi unaanza siku makumi tatu mbele ya uchaguzi na inamalizika saa makumi mbili na inne mbele ya uchaguzi.
Kampenyi ya uchaguzi kwa usikivu ungine, yaani utetezi wa uchaguzi kwa usikivu ungine, inajulisha kila mda ao wakati ambao vyama vya siasa na wakandidenti wanajijulisha, na kuweza pia kujulisha maoni yao na mipango yao. Mda huo hauchunguzwe na sheria kuhusu uchaguzi. Lakini, hatau zote zenyi kuelekea mippango ya hukumu ao katiba kuhusu ukingo wakila amtu,juu ya kuseana uwongo,kutusi, kushambulia heshima ya mwengine,ao kusukuma watu kwa chuki kati yaoao kuwasukuma kutenda maovu, sheria ya kupinga vitendo vile inapashwa kuheshimiwa.
Vyama vya siasa na wakandidenti wanapashwa zaidi na zaidi kutii mipangoiliyochuliwa na ambao waliisahihi kwa shiriki kwa uchaguzi mbali mbali..
” TUNAWEZA KUJUA KAMA NI NANI ANAPASHWA KUFANYA UTETEZI WA UCHAGUZI NA GINSI GANI HUENDA KUTENDEKA ? ”
* Karine, sheria kuhusu uchaguzi inamapatia kila kandidenti na kwakila chama cha siasanafasi na wakati wakufanya utetezi wake juu ya rn Nukta ya 29 ya sheria kuhusuucahaguzi inahakikisha kama mikutano ya uchaguzi huenda kufanyika kulinganana mipango iliyochukuliwa kwa mda uliopangwa.juu ya mikutano ya wote.N hiyo huenda kufanyika na vyama vya siasa na wakandidenti huru.
Mikutano na kampenyi ya uchaguzi ya kiserkali huenda kufanyika kwa uhuru katika eneolote la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, lakini kwa shurti hiyo, inafa walioanda mikutano ile wajulishe viongozi vya serkali sa 24 mbele ya kufanya mikutano yao.Wenyi kuanda mikutano ao waanadamanaji wa uchaguzi wanapshwa kulinda usalama ,ili mikutanao yao ifanyika katika hali ya kuheshimu mipango ya amani na ile ilichukuliwa na sheria Mda wote wa kampenyi , kutia picha aoa matangzo na vifa vingine vya utetezi juu ya uchaguzi kataika hali iliyokubaliwa na Cei , haikatazwe.Lakini kutia picha ao matangazo katka vyumba vya serkali haiuruhusiwe.
” KWA KUMALIZANI WANANI WENYI KUKATAZWA KWA KUFANYA KAMPENYI AO UTETEZI KISERKALI ? ”
* Karine,nukta 31 na 32 ya sheria kuhusu uchaguzi inakataza kila mtumishi waserkali, waendesha mastaki, waaskari jeshi na waaskari polisi, wataumishi wa ujasusi ,kushiriki kataika maandamano ya kisiasa,labda tuu wale waliomba ruhusa,ili waachwe huru kwamda fulani kwani wanatamani kufanya siasa, ao,pia wale waliojihuzuru. Inakatazwa pia kwa watu wale kutia matangazo, kugawanya vikartasi na maandiko mengine juu ya uchaguzi.
Tujue Karine Kakasi,kwa mwisho kama kiisha kumalizishwa kwa kampenyi ya uchaguzi yaani utetezi kiserkali, inakatazwa kugawanya siku ya uchaguzi, makartasi yenyi kutetea mtu fulani.Na pia inakatazwa kuvaa nguo ao mpira unao sura ao maandiko ya chama ao mkandidenti, ao tena kuwa na alama ya chama cha siasa fulaniaoa la kundi la kisiasa, ao tena sura ao picha ya viongozi vya chama mahali pa uchaguzi,hiyo inakatazwa kabisa.
Texte de SAMUEL KATSHAKrnTél. :00243998909787rnExt. :6961rnE-mail : [email protected] [email protected]
Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA