" Eneo la uchaguzi ni nini na ukubwa wake ni gani ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

“Eneo la uchaguzi ni nini na ukubwa wake ni gani?”

Eneo la uchaguzi ni mahali katika teritoria ya taifa ambako kura inapitikana.Ni mahali ambako kura ya kumchagua mwana bunge ao msimamizi wa madaraka ya serkali.
Eneo la uchaguzi ni eneo la umoja wa uchaguzi ambako hupekua kura.ya msingi.
Eneo la uchaguzi linalingana na nafasi moja ao nyingi kufatana na uchaguzi unaoandaliwa,wabunge ao wa uraisi.
Eneo la uchaguzi kwa uchaguzi wa wanabunge majimboni katika majimbo,ni mji ao teritoria- katika mji wa Kinshasa , eneo la uchaguzi ni mtaa yaani komini.
Idadi ya maeneo ya uchagauzi kwa kila bunge la jimbo ni-rn-wanabunge48 kwa amajimbo yrnyi kuwa na zaidi ya watu milioni mbili na elfu mia tanao wenyi walijiandikisharn- wanabunge 42 kwa majimbo yenyi kuwa kati ya watu milioni mbili na moja na milioni mbili na elfu mia tano wenyi walijiandikisharn-wanabunge 36 kwa majimbo yenyi kuwa na watu milioni moja mia tano na moja na milioni mbili waliojiandikisha.
-wanabunge 30 kwa majimbo, yenyi kuwa na watu waliojiandikisha milioni moja na moja na milioni moja na elfu mia tano.
Wanabunge 24 kwa majimbo, yenyi kuwa na watu waliojiandikisha,kati ya elfu mia tano na moja na milioni moja.
Wanabunge 18 wa majimbo , yenyi kuwa na wandikwa elfu mia tano ao chini.
Inafaa kujua kama daftari ya wakandidenti wa bunge la majimbo yanatolewa na chama cha siasa ao kundi la siasa.Wakandidenti pasipo chama cha siasa wanajijulisha wenyewe.
Kila kandidenti kwa bunge la jimbo anapashwa awe mkongomani, na awe na umri wa miaka 25 mpaka wakati anapojulisha kandidenti yake. Inafaa awe na uhuru wa haki zake za kisiasa na awe na hali ya mchaguzi ao kujitambulisha na kujiandikisha siku ile anajulisha kandidenti yake.

“Unayo maoni gani kuhusu uchaguzi unaoelekea maliwali wa majimbo na makamu wao?”

Maliwali na makamu wao wanachaguliwa kwa mda wa miaka mitano,ambayo huenda kuongezwa kwa mara moja na kura ya wanabunge la majimbo,wenyi kuwa ao hapana inje ya bunge la jimbo.Wanashimikwa katika madaraka na dikriti ya raisi wa jamuhuri na wanachaguliwa kwa daftari moja na wasimamizi na kwa kura ya uwingi kwa mara ya pili.
Uchaguzi wa maliwali na makamu wao unafanyika ,kama ni nyuma mno , siku 21 kiisha kushimikwa kwa chumba cha bunge la jimbo.

“Basi Dunia , utuelezee mengi kuhusu eneo la uchaguzi wa washauri wa miji mikuu.yaani conseillers urbains.
rnEneo la uchaguzi ya washauri wa miji mikuu ni mtaa,yaani commune.Kila mtaa unawakilishwa na washauri inne.Washauri hao wanachaguliwa na washauri wa mitaa kwa kura ya ukadiri kufatana na mdafatari yenyi kuwa wazi kwa sauti moja ya juu, kulingana na mpango ya yule mwenyi sauti nyingi, na kwa mda wa miaka mitano ,ya kurudilia .
Kiisha kuchaguliwa kwao , washauri huenda kuchagua wameya na makamu wao kwa uongozo wa miaka mitano, ya kurudilia kwa daftari ya kusimamiwa na kufatana na kura ya mwenyi kuwa na sauti nyingi kwa mara ya pili.. Tukiwa tuu katika nukta hiyo,tujulishe kama eneo la uchaguzi kwa washauri wa mitaa ni mtaa ,yaani commune.Washauri hao wa mitaa wanachaguliwa kwa kura ya wote kulingana na daftari ya wenyi sauti nyingi wanabaki Daftari ya wa wakandideti kwa ushauri wa mitaa inatolewa na chama cha siasa ao kundi la siasa. Wakandidenti wasio na chama cha siasa., yaani wakandidenti huru wanajitambulisha wenyewe binafsi.
Katika hatua hiyo, washauri wa mitaa watawachagua viongozi vya mitaa na makamu wao.
Tujue kama kandidenti yeyote kwa uongozo fulani, tangu wanabunge la majimbo mpaka wa bourgmestre yaani viongozi vya mitaa, anapashwa kupana kwa chumba cha Cei chenyi kupatikana mahali walipo maoni yao yenyi kuandikwa kufatana na mpango ulichukuliwa.Maoni yale yenyi kuandikwa yanapashwa kusahiliwa na wakandideti. Hao wanapshwa pia kuleta cheti cha kujitambulisha na kile kinachojulisha maisha yao, kuleta picha inne ndogo, alama ya chama ao ya kundi lao la siasa, sura yaani photocopie ya vyeti vyao vya uchaguzi,cheti cha kuzaliwa, cheti kinachojulisha kama walilipa pesa zilizolamishwa kunako sanduku ya serkali , inafaa pia walete barua ya kujulisha kama wakandideti walitumwa na vyama vyao vya siasa ao makundi yao ya siasa.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes CourtesrnTél. : 00243998909787rnE-mail :[email protected] [email protected]

Traduction en Swahili de DUNIA MUKUNDA