Kulizinduliwa siku ya kwanza tarehe makumi mbili na nane Novemba huko Bukavu kampeni ya chanjo ya kuzuia ugonjwa wa fievre jaune, huu unatokana na kuumwa na mbu. Ni mitaa ya afya tatu tu ya mjini ya Bukavu ambayo inahusika kwanza. Lakini lengo ni kuwachanja watu wote kuanzia umri wa miezi tisa hadi miaka makumi sita katika mitaa ya afya makumi tatu na ine ya Kivu Kusini. Fievre jaune ni nini? Je, kampeni hii ya chanjo itafanyika vipi? Daktari Joseph Matundanya, mratibu wa mkoa wa programu iliyoongezwa ya chanjo, PEV katika Kivu Kusini, anatoa maelezo yote katika mahojiano haya na Jean Kasami/sites/default/files/2022-12/021222-p-s-invitedrjoseph_matundanyapev_sud-kivu-00_web.mp3