" namna gani operesheni za uchaguzi huenda kufanyika, na kazi za washahidi na wachunguzi katika vyumba vya uchaguzi ni gani ? "

Fichier audio : téléchargez Flash pour écouter.

” Namna gani operesheni za uchaguzi huenda kufanyika, na kazi za washahidi na wachunguzi katika vyumba vya uchaguzi ni gani ? ”

* Naam,Karynne Kakasi,ulizo lako ni nzuri sana. Inafaa kwanza kujulisha kama uchaguzi,kulingana na maana yake tangu mwanzo ni sauti yenyi kupanwa na kila mtu mwenyi kuitwa ao kualikwa, ili atoe maoni yake juu ya jambo fulani. Ni kitendo amabacho kinawaruhusu warahiya wa inchi fulani ao wanamemba wa shirika fulani wanajulisha maoni yao kupitia uchaguzi ao kwa kuchukua hatua fulani.Kufatana na sheria sifuru sita,kistari sifuru, sifuru ya tarehe tisa mwezi wa tatu mwaka wa 2006, yenyi kuelekea matayarisho ya uchaguzi mbali mbali ,ya uraisi wa jamuhuri .ya wateule wa bunge la taifa,ya majimbo, ya miji mikubwa,ya makomini na ya malokaliti, katika jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Uchaguzi ni wa kipekee na hauwezwi kufanyika na mtu mwengine kwa jina la mwengine, ao kufanyika kwa njia ya barua.Kwa swali lenyi kuelekea namna gani huenda kufanyika, mpango wake ni mwepesi.Unafika pa chumba cha uchaguzi, pa kuingia unaonyesha cheti chako cha mchaguzi kwa wasaidizi wakiongozi wa chumba kile cha uchaguzi,hao watachungua kama jina lako linapatikana juu ya dafatari ya watakaochagua,katika chumba kile.Kiisha hapo ,kiongozi wa chumba cha uchaguzi atakupatia cheti cha uchaguzi.Kiisha unajielekeza mahali pa upekee yaani isoloir, hapo utakuwa mwenyewe kwa kuchagua, na hakuna hata mtu mmoja atakaye jua kama ulimchagua nani.Mahali pale pa upekee ao isoloir,utatia chapa ya kidole chako kikubwa juu ya eneo la yule ambaye unamchagua.Unakunja cheti cha uchaguzi kwa kufichika uliyemchagua. Kiisha hapo,unaondoka katika isoloir,ao mahali pa upekee na kujielekeza hivi kwenyi kunapatikana sanduku ya kutumbukiziamo vyeti vya uchaguzi, mbele ya washahidi,kwa kutumbukiza cheti chako ndani ya sanduku .
Nyuma ya hayo inasahihi mahali jina lako linapatikana juu ya madaftari ya wachaguzi walioandikwa kwa chumba kile cha uchaguzi.Ikiwa akama haujue kusahihi,unatia chapa ya kidole chako.Mbele ya kumrudishia mchaguzi cheti chake cha uchaguzi,presidenti wa chumba cha uchaguzi anampagaa wino juu ya kidole chake kikubwa ao juu ya kidole chochote cha mkono wake.

” Basi, Dunia Mukunda Milemba, tunaweza kuelewa kama kiisha uchaguzi,ni mpango gani ungine huenda kufata ? ”

* Karynne Kakasi,kufatana na sheria ya uchaguzi,kiisha uchaguzi kumalizika ni palepale,kiisha mda mfupi,ni mpango wa kupekua vyeti vilivyotumbukizwa ndani ya sanduku ndio utaanzishwa.Na mpango ule ni wa kuhesabu idadi ya vyeti, na wakujua hivi nukta za uchaguzi.Upekuaji wa vyati vya uchaguzi unafanyika mbele ya washahidi na wachunguzi wa taifa na wale wa kimataifa

” Dunia Mukunda Milemba,washahidi wa uchaguzi wauchaguzi wanao kazi gani katika vyumba vya uchaguzi ? ”

* Karynne Kakasi , inafaa tujue kama mshahidi kila mkongomani mwenyi kutumwa na kandidenti huru, na chama cha siasa ao kundi la siasa na anayekubaliwa na kutumwa na Cei kwa kuhuzuria mwenendo wa operesheni za uchaguzi. Anasahihi ripoti na anaandika po maoni yake na masito anayo kuhusu aliyeyaona.Mchunguzi wa uchaguzi ni kila mkongomani ao mgeni mwenyi kutumwa na shirika la taifa ao la kimataifa na anayekubaliwa na kutumwa na Cei, kwa kushiriki kwa mwenendo wa operesheni ya uchaguzi mbali mbali.Kuhusukazi yake, sheria akuhusu uchaguzi inahakikisha kamawashahidi na wachunguzi wauchaguzi wanahuzuria mipango yote ya uchaguzi na ya upekuaji wa vyeti vya uchaguzi,wanachungua uokotaji wa vyeti ndani ya sanduku na kuhesabiwa kwao, mpaka kufukia kwa idadi za nukta ya uchaguzi.Washahidi na wachunguzi wale hawapo wanamemba wa chumba cha uchaguzi na hawezi kushiriki pa mkutano wa kutatua shida fulani ao kuulizwa maoni yao.
Wanao haki ya kujulishwa msingi wa maoni ao matatizo na masito yenyi kuelekea mwenendo bora wa operesheni ya uchaguzi mbali mbali ,ni kusema maoni , masito na magumu yenyi kuandikwa ndani ya ripoti mbele ya kuifunga na kuituma. Karynne Kakasi, inafaa tujue kama washahidi wanalishwa na kuchukuliwa na wale waliowataja,lakini kwa upande wao wachunguzi hawachukuliwe maishani mwao mda wakazi zao wala na serkali ya Kongo kidemokrasia ,wala na komisheni huru ya uchaguzi.Ila usalama wao unakingwa na serkali .Inafaa kujua kama ukosefu wa wachunguzi katika chumba cha uchaguzi siyo jambo linaloweza kusababisha kura isikubaliwe,labda kama kutokuweko kwao kulifanyika kwa utashi wao na kwa shabaa ya kupinga sheria ya uchaguzi.

Texte de SAMUEL KATSHAKrnOndes Courtes 3è HeuresrnTél. : 00243998909787rnExt. : 6961rnE-mail : [email protected] [email protected]

Traduction Swahili de DUNIA MUKUNDA