Utofauti wa lugha ilionao Ituri ni utajiri unaopaswa kukuza kuishi pamoja na sio kuwa jambo linaloleta migawanyiko ndani ya jamii. Haya ni maneno ya Bagamba Arahali, profesa wa lugha na mtaalamu wa tabia za lugha. Ilikuwa katika hafla ya tarehe makumi mbili na moja Februari, Siku ya Kimataifa ya Lugha ya Mama. Katika mahojiano haya yaliyotolewa na Redio Okapi, Profesa Bagamba Arahali, anarejea umuhimu wa siku kama hiyo inayotolewa kwa lugha ya mama, lakini pia kwa utofauti wa lugha za Ituri, kama kiboreshaji cha amani. Anazungumza na Ezechiel MUZALIA.
/sites/default/files/2025-02/270225-p-s-invitebuniabagambaarahalilanguematernelle-00-web.mp3