Habari za siku ya pili jioni tarehe 23/07/2024
- Bwana Jean-Bosco Bahala, ameondolewa madaraki mwake kama kiongozi wa Mpango wa Kupokonya Silaha PDDRC-S. Ni kulingana na amri ya rais wa jamuhuri Felix Tshisekedi iliyotangazwa siku ya pili hii mjini Kinshasa.
- Kiongozi wa mtaa wa Fungurume, katika jimbo la Lualaba anakataza Wakaazi wa Fungurume na maeneo jirani kula samaki kutoka kando ya Mto Kelangile. Hatua hii inachukuliwa kufuatia kumwagiwa kwa bidhaa yenye sumu kwenye mto huu na gari kubwa liliopata ajali siku ya mungu iliyopita katika eneo hilo.
- Kikao cha tatu cha kongamano la kitaifa la huduma ndogo za fedha lilifunguliwa siku ya kwanza hapa mjini Kinshasa.
- Huko Kasai-Oriental, kuna ongezeko la bei ya mahindi katika masoko mbalimbali ya mji wa Mbuji-Mayi..
- Liwali wa mji wa Kinshasa anaomba wajumbe wa baraza la usalama jimboni kutokomeza kabisa hali ya kuluna, ujambazi na msongamano wa magari mjini Kinshasa.
- Katika jimbo la Ituri, vikosi vya pamoja vya jeshi la FARDC na Uganda vilishambulia maeneo kadhaa ya ADF siku ya mungu katika pori ya Mont HOYO, usulutani wa Walese Wonkutu kusini mwa mtaa wa Irumu.
- Jimboni Kivu ya kusini, Mahakama ya kijeshi ya Uvira iliyoketi huko Mboko katika mtaa wa Fizi iliwahukumu siku ya kwanza askari watatu wa Fardc kwa adhabu ya kifo .
- Liwali wa jimbo la Kongo-Central, Nkuanga Masuangi Bilolo Grace anaomba polisi na jeshi la Fardc kuimarisha juhudi zao ya kulinda raia na mali zao kwa heshima wa katiba.
- Jimboni Ituri, karibu visa mia mbili vya ajali za barabarani na vifo makumi mbili vimehesabiwa tangu mwanzo wa mwaka huu na polisi wa barabarani mjini Bunia.
- Katika jimbo la Kasai-Central , chama cha kutetea haki za watoto na wanafunzi, LIZADEEL inatoa wito kwa wazazi kuchukua hatua za kulinda watoto wakati wa matokeo ya mitihani ya serikali./sites/default/files/2024-07/230724-p-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3