Habari za siku ya kwanza jioni tarehe 22/07/2024
- Waziri mkuu Judith Suminwa anaomba wanamemba wa serikali kutumika kwa ukweli kwa ajili ya wanainchi ambao wanakuwa na matatizo mengi na kuatcha matendo mabaya sawa vile wizi wa pesa ya serikali. Alisema hayo siku kwanza hii wakati wa kikao cha serikali hapa mjini Kinshasa.
- Jimboni Kivu ya Kusini, liwali anasimamisha shughuli za uchimbaji madini kwenyi maeneo yote ya uchimbaji madini katika jimbo hilo. Jean Jacques Purusi pia anawasimamisha kazi wakuu wote wa offisi ya kukusanya mapato ya jimbo , PMR Kivu Kusini.
- Kuhusu hatua hizi, .shirika la kiraia jimboni Kivu ya Kusini linamhimiza liwali kuzingatia mapendekezo na matakwa yaliyotolewa na Asasi za Kiraia lakini pia na bunge la jimbo.
- Katika jimbo la Kasai ya Mashariki, liwali wa jimbo anatangaza kwamba mradi mmoja tu kati ya mitano unaofadhiliwa na shirika FPI ndio unatekelezwa vyema na kampuni yaliyochaguliwa kufanya kazi
- Msongamano mkubwa wa magari uanooonekana kwa kuingia mji wa Matadi: Meya wa mji huu anakataza kuweka biashara kando ya barabara.
- Hakuna umeme kuanza siku ya kwanzaa hii mjini Kalemie.Kufuatana na hiyo, Kwa sasa, REGIDESO/Kalemie haiwezi kuwapatia wakazi maji ya kunywa.
- Waandishi wa habari mjini Goma walisheherekea siky ya kwanza hi siku kuu ilimwenguni wa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini: kulikuwa mzozo wakati wote wa siku ya kwanza hii asubuhi katika eneo la Wakimbizi la Rusayo, mtaani Nyiragongo kufuatana na mauaji ya kijana mmoja na mtu aliyevaa vazi za kijeshi za FARDC.
- Huko Ituri, waasi wa ADF ambao wanakimbia oparesheni za pamoja za majeshi za Kongo FARDC na Uganda UPDF katika mtaa wa Irumu wanaendelea kusonga mbele kuelekea Mambasa./sites/default/files/2024-07/220724-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3