Habari za siku ya tano jioni tarehe 19/07/2024
- Afisa mjumbe makamu wa liwali jimbo la Kivu ya kaskazini anaomba serikali ya Kongo na Baraza la Usalama la Marekani kukomesha kwa hakika mapigano kati ya jeshi la Kongo na waasi wa m23/RDF kupitia njia za kisiasa.
- Umoja wa Ulaya unakaribisha upanuzi wa siku kumi na tano wa usitishaji vita wa kibinadamu ambao unaona "ni muhimu sana" mashariki mwa Kongo
- Huko Ituri, liwali wa jimbo anaomba makundi yenye silaha kukomesha ukiukwaji wote wa haki za binadamu dhidi ya wakazi katika mikoa ya madini , na kuheshimu makubaliano mbalimbali ya amani yalitiwa saini na viongozi wao.
- Makundi kadhaa ya wanaodaiwa kuwa majambazi yaliwasilishwa jana siku ya inne mjini Lubumbashi kwa liwali makamu wa jimbo la Haut Katanga na kamishna wa polisi jimboni.
- Jimboni Kwilu, liwali wa jimbo , Félicien Kiway Mwadi anasikitishwa na ukosefu wa usalama unaosababishwa na Mobondo katika eneo la Bagata, ukosefu wa usalama ambao unatoka katika mtaa wa Kwamouth huko Mai-Ndombe.
- Katibu mkuu wa chama cha kisiasa UDPS Augustin Kabuya anajibu kwa wale waliosema jana kwamba wamemuondoa kwenye kiti chake. Anasema kwamba ana saini na anaweza kuwafukuza wakorofi. Kwa hiyo anaota wito wa utulivu.
- Watu wanaoishi na ulemavu wanamshutumu mwabunge Eliezer Ntambwe siku ya inne hii kwa kutaka kumvuruga waziri wao.
- Kwa upande wake mwanabunge huyo Eliezer Tambwe anatupiliya mbali kabasi madai yote haya yanaotolewa dhidi yake .
- Shirika la Afya duniani OMS linatangaza kwamba kwa miaka kumi iliopita, viwango vya vifo kutokana na ajali za barabarani vimeongezeka kwa kiasi kikubwa barani Afrika, na kusababisha vifo vya takriban watu elfu miya mbili na makumi tano katika barabara za bara Afrika mwaka wa elfu mbili makumi mbili na mmoja pekee./sites/default/files/2024-07/19072024-s-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3