Habari za siku ya tano asubuhi tarehe 08/12/2023
- Katika jimbo la Kivu Kaskazini, mji wa Mushaki, katika mtaa wa Masisi, unachukuliwa na waasi wa M23, kulingana na duru kadhaa.
- Kuhusu hali ya usalama Kaskazini mwa nchi, mkuu wa MONUSCO Bintou Keita anasema ana wasiwasi na kuhusu mapigano mashariki mwa inchi . “
- Matakwa ya M23 ni kwamba kusiwe uchaguzi katika baadhi ya maeneo ya jimbo ya Kivu Kaskazini tarehe makumim mbili mwezi na mwaka huu tunao. Hii ni maono kutoka kwa mwanabunge wa taifa Juvénal Munubo
- Jimboni Kivu ya Kaskazini- Siku, moja kabla ya kumalizika kwa muda wa kazi ya kikosi cha EAC kilichotumwa katika eneo la Masisi na Rutshuru, vikosi vingi vinavyounda kikosi hiki tayari vimejiondoa isipokuwa kikosi cha Uganda ambacho bado kinaonekana Rutshuru.
- Kuhusu Uchaguzi wa Rais, wagombea, Moise Katumbi Chapwe nambari 3 pamoja na Mchungaji Abraham Ngalasi namba kumi na sita, waliendesha kampeni zao za uchaguzi katika eneo la Bandundu Kubwa.
- Jimbobni Kivu ya Kusini, Wilaya ya Kalehe, Offisi ya kuaanda uchaguzi CENI ilifika siku ya tatu huko Bunyakiri ilikupeleka vifaa via uchaguzi.
- Tume ya Uchaguzi CENI inaendelea na operesheni ya kutowa vieti kwa mashahidi kutoka vyama vya siasa, makundi pamoja na wagombea Huru./sites/default/files/2023-12/081223-journalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3