Habari za siku ya inne jioni tarehe 07/12/2023
- Katika jimbo la Kivu Kaskazini, mji wa Mushaki, katika mtaa wa Masisi, unachukuliwa na waasi wa M23, kulingana na duru kadhaa.
- Kuhusu hali ya usalama Kaskazini mwa nchi, mkuu wa MONUSCO Bintou Keita anasema ana wasiwasi na kuhusu mapigano mashariki mwa inchi . “
- Jimbon Kivu ya Kaskazini- Siku, moja kabla ya kumalizika kwa muda wa kazi ya kikosi cha EAC kilichotumwa katika eneo la Masisi na Rutshuru, vikosi vingi vinavyounda kikosi hiki tayari vimejiondoa isipokuwa kikosi cha Uganda ambacho bado kinaonekana Rutshuru.
- Huko Ituri, miili sita mipya iligunduliwa siku ya tatu na askari wa FARDC waliokuwa kwenye doria za kivita karibu na kijiji cha Mayuwano katika usulutani wa Babila Babombi, karibu kilomita makumi tatu na mji wa Mambasa kwenye barabara ya Makeke.
- Mjini Kunshasa, Wafungwa makumi tano na watatu kutoka gereza kuu la Makala walihamishwa siku ya inne hii hadi kambi ya Luzumu iliyoko jimboni Kongo Central.
- Kuhusu Uchaguzi wa Rais, wagombea, Moise Katumbi Chapwe nambari 3 pamoja na Mchungaji Abraham Ngalasi namba kumi na sita, waliendesha kampeni zao za uchaguzi katika eneo la Bandundu Kubwa.
- Jimbobni Kivu ya Kusini, Wilaya ya Kalehe, Offisi ya kuaanda uchaguzi CENI ilifika siku ya tatu huko Bunyakiri ilikupeleka vifaa via uchaguzi.
- Tume ya Uchaguzi CENI inaendelea na operesheni ya kutowa vieti kwa mashahidi kutoka vyama vya siasa, makundi pamoja na wagombea Huru.
- Shirika wa mashauriano ya kiraia ya Lualaba unanotowa tahadhari kuhusu uchaguzi wa tarehe tarehe makumi mbili mwezi wa kumi na mbili.
- Wafanyakazi wa serikali katika jimbo la Maï-Ndombe, hasa wale walio katika mji wa Inongo, wametumika bila malipo kwa miezi miwili, ambayo ni mwezi wa kumi na wakumi na moja ./sites/default/files/2023-12/071223-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3