Habari za siku ya tano jioni ya tarehe 23/06/2023
- Maaskofu wa Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo CENCO Jamuhuri wanaalika wakongoami wote kuwa makini . Pia wanashutumu ukosefu wa usalama na kutokuvumiliana kisiasa miezi michache kabla ya uchaguzi
- Amri mpya ya kutokutoka nje ilitolewa katika jimbo lote la Kwango kila siku kuanzia ya mbili za usiku hadi saa kumi na mbili za asubuhi.
- Mkutano ya mashirika inne inapangwa kufanyika siku ya pili ijayo mjini Luanda katika inchi la Angola kuhusu mzozo kati ya Jamuhuri yaKidemokratia ya Kongo na Rwanda.
- Shirika lisilo la kiserikali la Journaliste en danger kwa kushirikiana na internews waliandaa kikao ya uchunguzi ya mbinu za ufuatiliaji na taratibu za ulinzi wa wapashahabari.
- Jimboni Ituri, mbuga la wanyama la Okapi linalaani upotevu wa zaidi ya hekta mia nne za nafasi yake kufuatana na shughuli za kibinadamu.
- Katika jimbo la Maniema, Meya wa mji wa Kindu alianza jana siku ya inne huko Kindu kazi yakubomoa majengo yasiyoheshimu kanunu.
- Jimboni Kivu ya Kusini, zaidi ya wanafunzi makumi inne kutoka Kalehe hawajui jinsi ya kufanya mitihani katika vyuo vikuu vyao vya Bukavu.
- Katika jimbo la Kwilu, zaidi ya walimu makumi kenda wa shule kumi na moja za msingi za mji wa Bandundu wanashutumu kutolipwa kwa malipo yao kwa muda wa miezi sita ambayo ni franga elfu makumi tano yakikongomani pamoja na garama za uendeshaji za shule zao ./sites/default/files/2023-06/230623-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3