Habari za siku ya inne jioni tarehe 22/06/2023
- Mjini Matadi katika jimbo la Kongo Central, watu wengi wanastutumu kabisa ukosefu wa utulivu na amani katika bunge la jimbo hilo. Hiyo baada yakuondoshwa madarakani kwa Kiongozi wa bunge pamoja na mwandishi makamu siku ya pili iliyopita.
- Kuhusu Uchaguzi unaoandaliwa mwaka huu. Katika jimbo la Kwilu, tume ya kitaifa ya haki za binadamu, CNDH inawahimiza wanawake wa jimbo hili kwa ujumla na wale wa mji wa Bandundu kugombeya ku ubunge wa kitaifa na hata jimboni.
- Wanawake walizungumza kuhusu mchango wao kwa kuzuia migogoro, na kuimarisha amani nchini Jamuhuri yakidemokratia ya Kongo.
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, katika mtaa wa Masisi, kundi kubwa la wakimbizi limeonekana kwa siku chache huko Kitshanga, usulutani ya Bashali Mokoto kaskazini mwa eneo mtaa huo .
- Katika jimbo ya Kivu ya Kusini, Mbuga la wanyama ya Kahuzi Biega inaonya kuhusu kuwepo kwa watu wenye silaha kwenye eneo lake.
- Jimboni Ituri, wakimbizi wa vita makumi kenda kutoka eneo la Kigonze mjini Bunia na Kasenyi, kilomita makumi tano na tano kutoka Bunia, walifunzwa kutengeneza sabuni na kushona .
- Mtaani Beni, shule makumi mawili za msingi katika tarafa ya Elimu (EPST) ya mtaa wa Oicha zimepewa majengo na vifaa vya mafunzo .
- Wanabunge, maseneta na mashirika yote ya serikali na yasiyo ya serikali yaliyohusika na maswala yakupiganisha walizungumza siku ya tatu huko Zongo jimboni Kongo Central kuhusu Jinsi ya kuimarisha sheria kwa ajili yakupihanisha rushwa inchini Jamuhuri yakidemokratia ya Kongo./sites/default/files/2023-06/220623-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3