Habari za siku ya tatu jioni tarehe 21/06/2023
- Seneta Augustin Matata Ponyo Mapon anashutumu utumizi wa haki na mmamlaka ili kumuondoa ku uchaguzu unayopangwa kufanyika mwezi wa kumi na mbili mwaka huu
- Chama cha kisiasa Ensemble pour la Republique inashutumu na kulaani kile inachoeleza kama kutekwa nyara kwa Franck Diongo, kiongozi wa chama cha siasa cha Mouvement Lumumbiste Progressive, MLP.
- Maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya inne hii jimboni Ituri ili kuweka shinikizo kwa serikali ya Kongo na Umoja wa Mataifa hayatafanyika tena.
- Vikosi vya pamoja vya jeshi la Fardc-Uganda vimepanga kuimarisha operesheni ya kuwasaka waasi wa ADF katika eneo la magharibi mwa barabara ya taifa namba inne katika eneo mtaa wa Irumu.
- Wakati wa mkutano ililoandaliwa wikendi iliyopita katika Kambi ya Kokolo hapa mjini Kinshasa, Mkuu wa jeshi la FARDC Luteni Jenerali Christian Tshiwewe, aliwaomba wanajeshi kuwa wana hekima na busara, akisisitiza haswa nidhamu ambayo inapaswa kuwa ya askari yeyote.
- Mtaani Kalehe tuzungumze kuhusu Muendelezo wa kazi ya kufungua upya barabara ya kitaifa namba mbili Bukavu-Goma kati ya Bushushu na Nyamukubi. Ingawa inaweza kufikiwa na pikipiki, sehemu hii bado haipitiki kwa magari.
- Tarehe makumi mbili mwezi wa sita ya kila mwaka, ulimwengu unasherhe siku kuu ya Wakimbizi. Ni kwajili ya kuongeza ufahamu katika jamii kuwasaidia wale watu ambao wameiacha nchi yao kutafuta hifadhi kwingine.
- Marekebisho ya hali ya mahakimu ndio kiini cha mazungumzo huko Zongo kati ya wanabunge , maseneta, Baraza la Juu la Mahakama, Wizara ya Sheria na mashirika ya kiraia./sites/default/files/2023-06/210623-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3