Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni tarehe 11/05/2023

  • Jimboni Ituri, wanafunzi mia moja  kutoka mtaa wa  Djugu waliweza kufanya  mitihani ya kwanza ya serikali kupitiya   msaada wa  askari wa MONUSCO.
  • Katika jimbo la Maindombe, mitihani ya  kwanza ya serikali ya mwaka huu  imepangwa kwa sehemu katika mtaa wa Kwamouth. Wanafunzi kadhaa hawakushiriki kutokana na hali mbaya  ya usalama ambayo imesalia hapo.
  • Jimboni Kivu ya Kusini, kuhusiana na ajali ya mafuriko ya nvua  ya Kalehe, serikali la jimbo  inatoa wito wa usaidizi wa  jumla kwa ajili ya waathiriwa.
  • Siku bila kazi mjini Uvira katika jimbo la Kivu ya Kusini… Karibu  waandamanaji elfu moja, wakiwemo wavuvi, akina mama wanauzisha  samaki kutoka ziwa  na watu  wengine, waliandamana  siku ya siku ya inne hii .
  • Kufungwa kwa uvuvi katika nchi nne za pembezoni ni moja ya hatua nyingine nyingi zilizochukuliwa katika  mradi wa LATAFIMA, mradi wa usimamizi wa Uvuvi wa Ziwa Tanganyika.
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, eneo la afya la Lubero na lile la Mangurijipa hazina gari lakuchukuwa wagondjwa kwa dharura.
  • Katika jimbo la Kivu ya  Kaskazini, tuwajulishe kwamba zaidi ya wanawake mia mbili wahami   wamefaidika na huduma salama ya uzazi katika eneo la Bulengo kwa muda wa siku makumi tatu zilizopita
  • Majenerali wawili wa jeshi na polisi wafikishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Kijeshi mjini Kinshasa./sites/default/files/2023-05/110523-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3