Journal Soir

Habari za siku ya inne jioni 

  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, sehemu ya mji  wa Kibumba inachukuliwa  tena, siku ya tano hii na jeshi la Kongo
  • Jeshi la Uganda linatayarisha kutuma  wanajeshi wengine  nchini Kongo  kwa niaba ya kikosi  cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
  • Watu sita akiwemo mwanamke mmoja walifariki kwa  kupigwa risasi na wengine wanne kujeruhiwa vibaya .
  • Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, msimamizi wa huduma  ya itifaki yani protocoli  wa gavana wa kijeshi amefungwa siku ya tano hii mjini Kinshasha.
  • Serikali la Jimbo la Kwilu ilikabizi  rasmi jana siku ya inne  vifaa vya shule na bidhaa nyingine kwa watoto wahama , wahanga wa ukatili wa mtaa wa  Kwamouth, walioandikishwa katika shule za Bandundu, mji mkuu wa jimbo hili.
  • Mjini  Beni, suala la vita dhidi ya rushwa  lilikuwa lilizungumziwa wakati wa kikao cha kujadiliana leo hii siku ya tano kilichoandaliwa na shirika lliitwao bunge la vijana kwa ushirikiano na offisi ya masuala ya kisiasa ya MONUSCO.
  • Bunge la jimbo la  Lualaba lilichaguwa wakati wa kikao cha jana siku ya inne  azimio linalomuruhusu  mwendesha mashtaka wa umma kufungua kesi dhidi ya liwali  Richard Muyej na kufunguliwa kwa  kesi zidi ya mwanabunge jimboni Louise Mueleshi kwa wizi  wa pesa zilizokusudiwa kuunga mkono mradi wa kilimo wa mwaka elfu mbili na kumi na kenda – elfu mbili na makumi mbili .
  • Jimboni Ituri, wafungwa watatu wa gereza kuu la Mambasa walifariki jana siku ya tatu katika hospitali kuu ya eneo hili iliyoko kilomita mia moja makumi sita na tano  kusini-magharibi mwa Bunia./sites/default/files/2022-11/181122-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3