Journal matin

Habari za siku ya pili asubuhi 

  • Katika eneo la Walikale jimboni  Kivu ya Kaskazini, wakazi wa vijiji vingi vya tabaka Ikobo wamekimbiya makaazi yao tangu asubuhi ya siku ya kwanza hii.
  • Katika jimbo ya Kivu ya Kaskazini, mkusanyiko wa vijana wanaojitolea, unaoitwa "Goma Actif" inajitokeza kupitia vitendo vya Kibinadamu kwa ajili ya wakimbizi  kutoka Rutshuru ambao wako Kanyarutchinya.
  • Huko Ituri, makumi ya waandishi wa habari na watendaji wa shirika la raia walinufaika na mafunzo  siku ya sita na siku ya kwanza hii juu ya mapambano dhidi ya taarifa ya nia mbaya na matamshi ya chuki pa Mahagi na Aru-centre maeneo yanayopatikana kwa kilomita mia moja makumi mnane na mia tatu kaskazini kutoka Bunia.
  • Huko Kasaï-Oriental, bei za vyakula vingi zimepanda huko Mbuji Mayi.
  • Bei za vyakula vyote na zile za mahitaji ya msingi zilimepanda katika masoko ya jiji hilo.
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, bei ya tiketi ya usafiri kwa gari imeongezeka katika mashirika ya uchukuzi yanayotumia barabara ya Butembo-Goma.
  • Katika jimbo la Tshopo, mpango mkakati wa sekta mbalimbali wa malisho mabaya ulioandaliwa tangu mwaka elfu mbili kumi na tisa  wakati wa mkutano mkuu wa kilimo na malisho unakabiliwa na tatizo la kutekelezwa.
  • Huko Equateur, mfumo wa mashauriano wa mashirika ya kiraia wa mkoa ulionyesha wasiwasi wikendi hii kuhusu hali ya kuwa mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo hauendi.
  • Katika mkoa wa  Kongo centrale, ofisi ya polisi ilivamiwa na raia, baada ya  kifo cha kijana mdogo mchana wa siku ya Jumapili tarehe sita Novemba  mwaka tunao katika kituo cha polisi, kilicho katika manispa Kinzaumvuete, katika tarafa la Sekebanza./sites/default/files/2022-11/081122-p-s-journalswahilimatin-00_web_.mp3