Journal Soir

Habari za siku ya pili jioni tarehe 06/12/2022

  • Awamu ya tatu ya mchakato wa amani mashariki mwa DRC imefungwa siku ya pili hii.
  • Tukio lililotokea siku ya kwanza mjini Nairobi katika awamu ya tatu ya mchakato wa amani mashariki mwa DRC kuhusu suala la pesa iambayo wangenufaiaka wanachama wa makundi yenye silaha, halikuhusu serikali ya Kongo, bali ukatibu wa EAC.
  • Katika Kivu Kaskazini, hali imekuwa shwari tena karibu na mji wa  Kitshanga, unaopatikana kati ya tarafa za Ruthuru na Masisi.
  • Wanawake wa Kivu Kaskazini, kutoka jamii zote za jimbo hili, wanapaza sauti zao kushutumu kile wanachoeleza kama mauaji ya kimbari ya wakazi wa Kongo huko Kishishe na Kisharu tarafani Rutshuru.
  • Habari kuhusu Ukosefu wa usalama katika tarafa la Bagata, jimbo la Kwilu, shambulio jipya la washambuliaji wenye kumiliki silaha lilisababisha vifo vya watu kumi na tatu usiku wa kuamkia siku ya pili hii tarehe sita Desemba, katika kijiji cha Kingala Matele kilicho katika sekta ya Wamba, jirani na sekta ya Bukanga-Lonzo katika jimbo la Kwango.
  • Huko Ituri, watu wawili waliuawa usiku wa kuamukia siku ya pili hii na watu wasiojulikana wenye silaha huko Nzere 2 kwa umbali wa takriban kilomita kumi kutoka Bunia.
  • Huko jimboni Kivu Kusini, Chama cha Wanawake wa Vyombo vya Habari, AFEM kinaongeza ufahamu kuhusu matukio ya unyanyasaji wa ndani ya ndoa katika kukuza haki za wanawake.
  • Miporomoko ya ardhi kumi na tano, yanatishia Kata Plateau 1 inayojulikana kwa jina maarufu la Chad, katika manispa Mont-Ngafula kupita eneo kunako wakazi wa UNIKIN./sites/default/files/2022-12/06122022-p-s-jiournalswahilisoir-00_web.mp3