Habari za siku ya pili jioni
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, mapigano makali yaliendelea hadi mwanzo wa jioni ya siku ya pili kati ya wanajeshi wa FARDC na waasi wa M23 kaskazini mwa mtaa wa Nyiragongo.
- Jimboni Kivu ya Kasakazini, tuwajulishe kwamba Upatikanaji wa maji ya kunywa ni hitaji kubwa ya wahami . Shirika ya ubeljiji ya Medecions sans frontieres tayari ilikuwa ikipeleka maji ya kunywa huko Kanyaruchinya kwa ajili ya wahanga wa mlipuko wa mlima wa moto na jamii .
- Katika jimbo la Kwilu, hali ya maisha ya wahami ni mbaya katika mtaa wa Bagata.
- Offisi la Seneti lilianza siku ya kwanza uchunguzi wa sheria ya kupiganisha rushwa , ufadhili wa ugaidi na kuenea kwa silaha za maangamizi makubwa.
- Jimboni Kwilu, tuwajulisha kwamba kunaonekana siku hizi ukosefu ya mazao ya kilimo na kusababisha ongezeko la bei ya bizaa hiyo kama mahindi na mihogo kwenye soko la mji wa Kikwit.
- Mtaa wa Lubudi jimboni Lualaba haina umeme kwa muda wa miezi miwili. Matokeo yake ni kwamba shughuli za kibiashara haziendeshwa vizuri.
- Jimboni Kasaï ya mashariki, huko ambako mji wa Mbuji-Mayi hivi karibuni itaweza kufaidika na kituo cha umeme unatolewa na jua wa megawati nane ili kusaidia shirika la Regideso kwa kuboeresha utowaji wa maji ya kunywa.
- Katika jimbo ya Maniema, mkurugenzi jimboni ahusikaye na elimu ya Maniema ya kwanza anaendelea na kampeni yake ya kupiganisha matendo mabaya katika shule na ofisi yakusimamiya shule jimboni humo./sites/default/files/2022-11/151122_-p-s-kinjournalswahilisoir-00_web.mp3