Habari za siku ya tatu asubuhi
- Liwali wa jimbo la Kivu ya Kaskazini anatoa wito kwa wakaaji wa Goma kutulia na kuwa waangalifu.
- Katika Jimbo hilo la Kivu ya Kasakazini, upatikanaji wa maji ya kunywa ni hitaji kubwa ya wahami .
- Katika jimbo la Kwilu, hali ya maisha ya wahami ni mbaya katika mtaa wa Bagata.
- Jimboni Kwilu, kunaonekana siku hizi ukosefu ya mazao ya kilimo na kusababisha ongezeko la bei ya bizaa hiyo kama mahindi na mihogo mjini Kikwit.
- Mtaa wa Lubudi jimboni Lualaba haina umeme kwa muda wa miezi miwili. Matokeo yake ni kwamba shughuli za kibiashara haziendeshwa vizuri.
- Jimboni Kasai ya mashariki,chama cha kifeza cha wanawake wa Afrika mjini Mbujimayi, MUFFA kwa kifupi, kilipewa jana siku ya pili dola laki moja, kutoka kwa shirika Kemesha, ambao inakutanisha mashirika mengine ikiwemo shirika Widal, Pierrette Bemba, Suzane Tshimwanga , MUFFA Mbuji Mayi mbele ya wanawake kadhaa wanamemba wa chama hicho.
- Jimboni Maniema, mkurugenzi jimboni ahusikaye na elimu ya Maniema ya kwanza anaendelea na kampeni yake ya kupiganisha matendo mabaya katika shule ya jimbo hilo./sites/default/files/2022-11/161122-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3