Habari za siku ya pili asubuhi
- Jimboni Kivu ya Kaskazini, mapigano yalifanyika jana siku mzima kati ya wanajeshi wa FARDC na waasi wa M23 kwenye pande mbili katika maeneo ya Rutshuru na Nyiragongo.
- Majadiliano ya awali ya mchakato wa amani wa Nairobi ya tatu: rais wa zamani wa Kenya aliyechaguliwa kuwa mpatanishi wa mchakato wa Nairobi na jumuiya ya Afrika ya Mashariki, alipokeya jana viongozi wa kisiasa wa inchi la Kongo Kongo na wawakilishi wa jumuiya tofauti kutoka Kivu ya Kaskazini, Kivu ya Kusini na Ituri.
- Habari kuhusu mzozo uliopo mjini Kinshasa kuhusu vikwazo vya silaha: wakati baadhi ya vyama vya siasa na vikundi vya raia vikipanga kuandamana dhidi ya Jumuiya ya Kimataifa kuhusu suala hilo, waziri ahusikaye na Mambo ya Nje amewaonya wananchi dhidi ya hatua zozote zitakazomsaidia adui wa Kongo. Katika mahojiano na Radio Okapi kutoka Luanda nchini Angola aliko, Christoph Lutundula anafasiria tena matamshi yake yaliyotafsiriwa vibaya sikun ya tano iliyopita kuhusu kuzuiwa kwa inchi kupata silaha. Kulingana naye inchi ya Kongo haiko tena chini ya vikwazo rasmi.
- Katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, eneo la afya ya Nyiragongo linatangaza kuenea kwa visa vya malisho mbaya katika maeneo mbalimbali ya wahami . Malisho mbaya hiyo huathiri zaidi watoto kutoka miezi sita hadi miezi makumi tano na kenda pamoja na wajawazito.
- “Kisukari: kuelimisha ili kulinda maisha yajayo” hii ndiyo ndiyo mada ya sherehe ya siku kuu duniani ya kupinga ugonjwa huu mwaka huu inayosherekewa kila tarehe kumi na inne mwezi wa kumi na mmoja .
- Katika jimbo la Kivu Kusini, maporomoko ya udongo yamesababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi mmoja vibaya katika mji wa Bukavu.
- Kunaripitiwa Vifo viwili kufuatia kutoroka kwa wafungwa wa gereza kuu la Gbadolite siku ya mungu . Viongozi wanasikitika kwamba zaidi ya wafungwa makumi mnane walifanikiwa kutoroka katika gereza hiyo ambayo haina vyoo bora.
- Wizi wa kila mara wa viombo via SNCC kwenye sehemu ya reli ya barabara ya Kindu – Kongolo – Kabalo katika jimbo la Tanganyika. Ni Kiongozi wa kituo cha SNCC huko Kongolo ndio alitangaza habari siku ya mungu .
- Kuwasili Mbuji-Mayi jana hii, huko Kasaï-Oriental, kwa ujumbe wa Mfuko ya Kitaifa kuhusu masuala ya pori /sites/default/files/2022-11/151122-p-s-kinjournalswahilimatingraceamzati-00_web.mp3.