Habari za siku ya inne asubuhi
- Hali ya mafuta ya gari pa Kinshasa na wasiwasi huu wa wakaaji wa Kinshasa kuhusu ukosefu unaowezekana katika siku zijazo.
- Kituo cha uchunguzi wa Volcano OVG cha Goma, kinatangaza kwamba kimegundua shughuli isiyo ya kawaida iliyorekodiwa siku ya pili kwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi katika maeneo yake ya uchunguzi ya Munigi na Kibati katika tarafa la Nyiragongo.
- Huko Nord Ubangi, takriban watu elfu kumi katika eneo la afya la Gumba-Lego, kilomita makumi ine na tano kutoka Yakoma-Kati, hawajui tena wapi pa kwenda ili kupata matibabu.
- Kongo Central ni jimbo la majaribio wa operesheni ya utambuzi wa kibayometriki kwa wafanya kazi wa serikali katika majimbo.
- Visa vingine viwili vya vifo vilirekodiwa siku ya kwanza tarehe kumi na siku ya pili tarehe kumi na moja mwezi wa kumi mwaka tunao miongoni mwa wakimbizi waliotoka Kwamouth, ambao kwa sasa wanaishi katika jimbo la Kwilu.
- Huko Mbuji Mayi, jimboni Kasai-Oriental, kuligunduliwa sehemu kubwa ya vifaa vya kupambana na malisho mabaya.
- Mchungaji Jean Omari Ramazani wa Kanisa la Eglise chrétienne pour toutes les nations, anayejulikana sana mjini humo, yuko mbele ya mahakama tangu hii siku ya tatu katika mahakama ya kijeshi ya Goma.
- Barua ya ombi ya Watu wanaoishi na Ulemavu, iliwasilishwa siku ya pili tarehe kumi na moja mwezi wa kumi , kwa Waziri Mkuu./sites/default/files/2022-10/13102022-p-s-journalswahilijeudimatin-00_web_.mp3