Habari za siku ya pili jioni tarehe 20/06/2023
- Mpinzani Franck Diongo, kiongozi wa chama cha kisiasa cha Mouvement Lumumbiste Progressive, MLP kwa kifupi , alikamtwa siku ya pili hii asubuhi na watu wenye silaha waliovalia vazi na kijeshi katika makutano ya barabara za Kabinda na Huilleries hapa mjini Kinshasa.
- Marekani inakaribisha ripoti ya mwisho ya Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
- Jimboni Ituri, shirika ya kiraia linaomba haki ya kijeshi kutoa hati za kukamatwa kwa wahusika wote wa uhalifu uliofanywa katika jimbo hili.
- "Endelea kutumaini kuishi ingawa mbali na nyumbani". Huu ndio ujumbe uliotumwa kwa wakimbizi wanaoishi mjini Goma na mwanamke mjasiriamali wa Kongo.
- Ulimwengu unasherehe siku ya pili hii, Siku kuu ya Wakimbizi. Huko jimboni Kivu ya Kusini, asilimia makumi kenda na sita ya wakimbizi wa Burundi katika jimbo hili, yaani zaidi ya watu elfu makumi inne wanapatikana katika eneo la Fizi pamoja na karibu ya waomba hifazi elfu tatu wa Burundi.
- Kulianzishwa siku ya kwanza huko Zongo katika jimbo la Kongo Central kikoa cha utetezi na mazungumzo juu yakupiganisha rushwa pamoja na na kuhusu kuboreshwa kwa sekta ya sheriya.
- Katika Jimbo la Kwilu, CENI inasema iko tayari kwa shughuli ya mapokezi ya wagombea wa ubunge kuanza tarehe makumi mbili na tano mwezio huu wa sita.
- Ilizinduliwa mnamo tarehe makumi mbilio mwezi wa sita , mwaka elfu moja miye kenda na makumi mnane na tatu na Rais wa zamani Mobutu, daraja iiitwao Pont Maréchal , huko Matadi, ilieneza miaka mwaka makumi inne siku ya pili hiii./sites/default/files/2023-06/200623-p-s-kinjournalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3