Journal Soir

Habari za siku ya tano jioni tarehe 16/06/2023

  • Katika jimbo la Ituri, watu kumi na watano waliuawa na nyumba kumi na mbili kuchomwa   wakati wa shambulio jipya la waasi wa ADF jana siku ya inne  katika eneo la Bandavilemba kusini mwa mtaa wa  Irumu.
  • Jimboni  Kivu ya Kusini, vijana wa mji wa Bukavu wamejianda kabisa  kwa ushiriki mkubwa katika mchakato  wa uchaguzi.
  • Kwa kutarajia Siku kuuu ulimwenguni  ya Mtoto wa Afrika inayosherekewa leo hii tarehe kumi na sita mwezi wa sita,  watoto wapasha habari wa Unicef ​​walifanya kampeni  siku ya inne iliyopita ya uhamasishaji juu ya ulinzi wa mazingira.
  • Jimbo la Kongo Central ni miongoni mwa majimbo yanayoshiriki katika kikoa  cha kumi na nane cha wiki ya madini ya Kongo ya Kidemokratia  ambayo inafanyika mjini Lubumbashi.
  • Jimboni  Tanganyika, mkuu  wa eneo la Kauwa katika usulutani  wa Bena Mambwe, mtaani  la Kongolo aliachiliwa jana na wanamungambo Maimai. Kulingana na msimamizi makamu wa mtaa wa  Kongolo, wa maimai  hawa kutoka emtaa wa Kabambare huko Maniema walishambulia eneo hili siku ya kwanza iliyopita .
  • Jimboni Kivu ya Kaskazini, hali ya usalama bado ni ya wasiwasi leo  hii katika maeneo kadhaa ya mtaa wa  Masisi.Ni jana ndio kikao cha kawaida cha mwezi wa tatu kilikomeshwa katika bunge la taifa ./sites/default/files/2023-06/160623-journalswahilisoirgraceamzati-00_web.mp3